跳到主要内容
Nelum
坦桑尼亚的法律

National Blue Economy Policy for 2024

颁布于 2024-04 · 文本截至 2026-10-01

以研究形式发布的公开法律与官方指引,不构成法律、税务或金融建议。

研究内容本身以英文撰写。标题和标签已翻译,调查结果和引文未翻译。

关于这部法律

语言
Swahili
类型
policy
国家
坦桑尼亚
主题
Fisheries and aquaculture, Sea, Water
关键词
marine fisheries, tourism, biodiversity, internal trade, international trade, freshwater fishes, sustainable development, sustainable use, data collection/reporting, integrated management, investment, research, enforcement/compliance, gender, good practices, governance, aquatic animals, irrigation, water resources management, ecosystem conservation, blue economy
类别
*

在哪里阅读

文本

所收录的法律原文,按条款排列。每个条款都有自己的链接。

  1. 1.0 UTANGULIZI ........................................................................................................... 1

  2. 1.1. HALI ILIVYO .......................................................................................................... 2

  3. 1.1.1 Uratibu wa shughuli za Uchumi wa Buluu ........................................................... 4

  4. 1.1.2 Matumizi ya Maeneo ya Maji ............................................................................... 5

  5. 1.1.3 Usimamizi katika eneo la Ukanda Maalumu wa Uchumi wa Bahari na Bahari Kuu ............................................................................................................................... 5

  6. 1.1.4 Uwekezaji ............................................................................................................ 6

  7. 1.1.5 Utafiti katika Rasilimali za Sekta za Uchumi wa Buluu ....................................... 7 SURA YA PILI ............................................................................................................... 8

  8. 2.0 UMUHIMU WA SERA, DIRA, DHIMA NA MALENGO YA SERA .......................... 8

  9. 2.1. Umuhimu wa Sera ................................................................................................. 8

  10. 2.2. Dira, Dhima na Malengo ya Sera .......................................................................... 8

  11. 2.2.1. Dira ..................................................................................................................... 8

  12. 2.2.2. Dhima ................................................................................................................. 8

  13. 2.2.3. Malengo ya Sera ................................................................................................ 9

  14. 2.2.3.1. Lengo Kuu.............................................................................................. 9

  15. 2.2.3.2. Malengo Mahsusi ................................................................................... 9 SURA YA TATU .......................................................................................................... 10

  16. 3.0 HOJA NA MATAMKO YA SERA .......................................................................... 10

  17. 3.1. Uratibu wa masuala ya Uchumi wa Buluu ........................................................... 10

  18. 3.2. Matumizi ya maeneo ya maji ............................................................................... 11

  19. 3.3. Uwekezaji ............................................................................................................ 11

  20. 3.4. Utafiti katika Rasilimali za Sekta za Uchumi wa Buluu ....................................... 12

  21. 3.5. Masuala Mtambuka ............................................................................................. 13

  22. 3.5.1. Jinsia ................................................................................................................ 13

  23. 3.5.2. Utawala Bora .................................................................................................... 14 SURA YA NNE ............................................................................................................ 15

  24. 4.0 MUUNDO WA KISHERIA ..................................................................................... 15 ii SURA YA TANO ......................................................................................................... 16

  25. 5.0 MUUNDO WA KITAASISI ..................................................................................... 16

  26. 5.1. Majukumu na Wajibu wa Wadau ......................................................................... 16

  27. 5.1.1. Ofisi yenye dhamana ya uratibu wa Uchumi wa Buluu .................................... 16 5.1.2. Ofisi yenye dhamana ya Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa .. 16

  28. 5.1.3. Ofisi yenye dhamana ya Mazingira na Muungano ........................................... 16 5.1.4. Ofisi yenye dhamana ya Menejimenti ya Utumishi wa Umma Utawala Bora ... 16

  29. 5.1.5. Ofisi yenye dhamana ya Mipango na Uwekezaji ............................................. 17 5.1.6. Ofisi yenye dhamana ya Uratibu wa shughuli za Serikali ................................ 17

  30. 5.1.7. Wizara yenye dhamana ya Fedha ................................................................... 17

  31. 5.1.8. Wizara za Kisekta ............................................................................................ 17

  32. 5.1.8.1. Wizara yenye dhamana ya Uvuvi ........................................................ 17

  33. 5.1.8.2. Wizara yenye dhamana ya Maji ........................................................... 17

  34. 5.1.8.3. Wizara yenye dhamana ya Kilimo na Umwagiliaji ............................... 18

  35. 5.1.8.4. Wizara yenye dhamana ya Nishati ...................................................... 18

  36. 5.1.8.5. Wizara yenye dhamana ya Uchukuzi................................................... 18

  37. 5.1.8.6. Wizara yenye dhamana ya Madini ....................................................... 18

  38. 5.1.8.7. Wizara yenye dhamana ya Maliasili na Utalii...................................... 18

  39. 5.1.8.8. Wizara yenye dhamana ya Viwanda na Biashara ............................... 18

  40. 5.1.8.9. Wizara yenye dhamana ya Ardhi ......................................................... 19

  41. 5.1.8.10. Wizara yenye dhamana ya Katiba na Sheria ..................................... 19

  42. 5.1.8.11. Wizara yenye dhamana ya Mambo ya Nje ........................................ 19

  43. 5.1.8.12. Wizara yenye dhamana ya Ulinzi....................................................... 19

  44. 5.1.8.13. Wizara yenye dhamana na Mambo ya Ndani ya Nchi ....................... 19

  45. 5.1.8.14. Wizara yenye dhamana ya Ujenzi ..................................................... 19 5.1.8.15. Wizara yenye dhamana ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ................. 19 5.1.8.16. Wizara yenye dhamana ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum............................................................................................... 20

  46. 5.1.8.17. Wizara yenye dhamana ya Sanaa na Michezo.................................. 20

  47. 5.1.8.18. Wizara yenye dhamana ya Afya ........................................................ 20

  48. 5.1.8.19. Mamlaka ya Usimamizi wa Bahari Kuu.............................................. 20 iii

  49. 5.1.8.20. Sekta Binafsi ..................................................................................... 20

  50. 5.1.8.21. Wadau wa Maendeleo ...................................................................... 21

  51. 5.1.8.22. Asasi za Kiraia .................................................................................. 21

  52. 5.1.8.23. Vyombo vya Habari............................................................................ 21

  53. 6.0 UFUATILIAJI NA TATHMINI ................................................................................ 21

  54. 7.0 HITIMISHO ............................................................................................................ 21 iv FASILI YA MANENO Fasili zilizotumika ni kwa madhumuni ya Sera ya Taifa ya Uchumi wa Buluu tu. Fasili hizi zinalenga kupunguza tofauti za tafsiri zinazoweza kujitokeza na kuongeza uelewa wa maana ya maneno mbalimbali yalivyotumika katika Sera hii. Bahari Kuu Eneo la bahari linalojumuisha Ukanda Maalumu Uchumi wa Bahari ya Tanzania na eneo la Bahari nje ya maili za bahari 200 ambalo halipo chini ya udhibiti wa Mamlaka ya taifa lolote ambapo mataifa yote yako huru kulitumia. Bioanuai Aina tofauti za viumbe hai kutoka vyanzo vyote ikiwa ni pamoja na nchi kavu, maji na ikolojia changamani ambayo ni sehemu ya mifumo ikolojia hiyo. Hii inahusisha tofauti za kibaiolojia baina ya jamii za viumbe na baina ya mifumo ikolojia. Mabadiliko ya Mabadiliko ya muda mrefu katika mifumo ya hali ya hewa na Tabianchi uso wa dunia kutokana na ongezeko la gesi joto baada ya kipindi kirefu cha angalau miaka thelathini (30). Mabadiliko ya hali ya hewa yanahusisha mwenendo wa mvua, joto, upepo, na unyevu unaojitokeza kwa kila siku. Maji ya Kitaifa Eneo la bahari la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lenye upana wa maili za bahari 12 linalopimwa kuanzia sehemu (alama) ya mwisho ya maji kupwa kuelekea baharini. Mifumo Ikolojia Maeneo yote ambayo yana jamii tofauti za viumbe hai kama vile mimea, wanyama, bakteria, kuvu, virusi, na protozoa pamoja na mazingira yao vikiwemo vitu visivyohai. Hii inajumuisha muingiliano na kutegemeana baina ya viumbe hao na mazingira yao. Rasilimali za Rasilimali zinazopatikana kwenye maeneo ya maji Uchumi wa Buluu yanayojumuisha bahari, maziwa, mito, mabwawa, maji chini ya ardhi, na maeneo oevu. Mfano wa rasilimali hizo ni madini, viumbe maji, gesi na mafuta. Teknolojia ya Teknolojia ya umwagiliaji inayotumia kiwango kidogo cha maji. matumizi banifu ya maji Uchafuzi wa Mabadiliko ya moja kwa moja au yasiyo ya moja kwa moja, ya Mazingira rasilimali za kimaumbile, hali ya joto, kikemikali, kibaiolojia, au sifa nyingine asilia, ambazo kwazo ni sehemu ya mazingira kwa kumwaga, kuachia, au kuweka taka; hivyo kuleta madhara kwa v matumizi yenye manufaa, kusababisha hali ambayo ni hatari kwa jamii kiafya, kiusalama au ustawi wa binadamu, au kwa wanyama, ndege, viumbe kwenye maji, au kwa mimea. Maeneo ya Maji Maeneo yaliyopo katika bahari, maziwa, mito, mabwawa na maji chini ya ardhi. Uchumi wa Buluu Shughuli za kiuchumi zinazohusu matumizi endelevu ya rasilimali za maji kwa manufaa ya jamii bila kuathiri mazingira. Ukanda Maalumu Ni eneo la bahari lenye upana wa maili za bahari 200 wa Uchumi wa linalopimwa kuanzia sehemu (alama) ambayo mpaka wa Bahari Bahari ya Kitaifa unaanzia kuelekea baharini. Ukuzaji viumbe Ufugaji na ukuzaji wa viumbe hai kwenye maji. maji Viumbe maji Mimea na wanyama wapatikanao katika maji bahari na maji baridi. vi VIFUPISHO CCM Chama Cha Mapinduzi MW Megawatt SADC Southern Africa Development Community (Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika) UKIMWI Upungufu wa Kinga Mwilini UVIKO-19 Ugonjwa wa Virusi vya Korona -19 VVU Virusi Vya Ukimwi DSFA Mamlaka ya Kusimamia Uvuvi wa Bahari Kuu TAFIRI Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania vii DIBAJI Uchumi wa Buluu ni dhana ambayo inachagiza ukuaji wa uchumi kupitia matumizi endelevu ya rasilimali za maji kwa kuzingatia uhifadhi wa mazingira na ushirikishwaji wa jamii. Tanzania imekuwa ikitekeleza shughuli za Uchumi wa Buluu kupitia sekta zenye mnasaba na Uchumi wa Buluu ambazo ni: Uvuvi; Maliasili na Utalii; Maji; Kilimo cha Umwagiliaji; Nishati; Uchukuzi; Madini; Uwekezaji, Viwanda na Biashara; na Uhifadhi wa Mazingira. Sekta hizi zimekuwa zikitekeleza shughuli za Uchumi wa Buluu kwa kuzingatia Sera, Sheria, Kanuni na Miongozo ya sekta husika. Pamoja na uwepo wa sera na sheria hizo, kumekuwepo na changamoto mtambuka zinazochangia Taifa kutonufaika ipasavyo na rasilimali za Uchumi wa Buluu zikiwemo: Kukosekana kwa mfumo jumuishi wa kitaasisi wa uratibu wa shughuli za Uchumi wa Buluu; Kukosekana kwa Mpango wa Matumizi wa Maeneo ya Maji; Uwekezaji usio wa kimkakati na fungamanishi katika matumizi ya rasilimali za Uchumi wa Buluu; na Uhaba wa utafiti na ujuzi katika matumizi ya rasilimali za Uchumi wa Buluu. Kwa kuzingatia hali hiyo, Serikali imeamua kutunga Sera ya Taifa ya Uchumi wa Buluu. Sera hii imebainisha masuala ambayo Serikali kwa kushirikiana na wadau, itayawekea mkazo zaidi ili kuweka mazingira mazuri ya kuhakikisha nchi inanufaika na fursa zitokanazo na rasilimali za Uchumi wa Buluu ili kukuza uchumi wa Taifa kwa maendeleo endelevu. Aidha, Sera hii itachangia katika kuwezesha nchi kufikia malengo ya maendeleo ya kikanda na kimataifa. Masuala muhimu yaliyozingatiwa na Sera hii ni pamoja na: Uratibu wa Shughuli za Uchumi wa Buluu; Matumizi ya Maeneo ya Maji; Usimamizi katika eneo la Ukanda Maalumu wa Uchumi wa Bahari na Bahari Kuu; Uwekezaji; na Utafiti katika Rasilimali za Uchumi wa Buluu. Ili kufanikisha utekelezaji wa Sera hii kwa ukamilifu, kunahitajika ushiriki wa wadau wote katika ngazi zote, ikiwemo Sekta Binafsi, Asasi za Kiraia na Washirika wa Maendeleo. Mwisho, napenda kuwashukuru wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine katika mchakato mzima wa kuandaa Sera hii. Aidha, ni matumaini yangu kuwa utekelezaji wa Sera hii utawezesha Nchi kunufaika ipasavyo na rasilimali za Uchumi wa Buluu zilizopo na hivyo kuchangia katika kukuza uchumi na kuongeza Pato la Taifa kwa maendeleo endelevu. Dkt. Selemani Saidi Jafo (Mb.) Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira viii SURA YA KWANZA

  55. 1.0 UTANGULIZI Uchumi wa Buluu ni dhana ambayo inachagiza ukuaji wa uchumi kupitia matumizi endelevu ya rasilimali za Uchumi wa Buluu kwa kuzingatia uhifadhi wa mazingira na ushirikishwaji wa jamii. Uchumi wa Buluu ulipewa msukumo mkubwa katika Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo Endelevu (Rio+20) uliofanyika Rio de Janeiro, Brazil mwaka 2012. Katika mkutano huo nchi za mwambao wa bahari ziliweka msukumo mkubwa wa kutambua matumizi endelevu ya rasilimali za bahari katika misingi ya kiuchumi, kijamii na kimazingira. Aidha, kufuatia Mkutano wa Kimataifa wa Uchumi wa Buluu Endelevu uliofanyika Nairobi, Kenya mwaka 2018, Viongozi wa Afrika walielekeza Umoja wa Afrika kuandaa Mkakati wa Uchumi wa Buluu. Mkakati wa Afrika wa Uchumi wa Buluu wa Mwaka 2019 umetambua shughuli zote za kiuchumi katika maji bahari, maji baridi na maji chini ya ardhi ambazo zinajumuisha maeneo makuu matano ya Uvuvi, ukuzaji viumbe maji na uhifadhi wa mifumo ikolojia ya maji; Usafirishaji, biashara, bandari, udhibiti, ulinzi na usalama baharini; Utalii wa fukwe na baharini, uhimilivu wa mabadiliko ya tabianchi, uhifadhi na usimamizi wa mazingira na uendelezaji wa miundombinu; Nishati endelevu, madini, teknolojia na ubunifu; na Sera, muundo wa kitaasisi, ajira, kupunguza umaskini pamoja na ugharamiaji. Kutokana na umuhimu wake, Uchumi wa Buluu umejumuishwa katika mipango na mikakati ya maendeleo ya kikanda na kimataifa kama vile Dira ya Jumuiya ya Afrika Mashariki 2050; Mpango Mkakati wa Maendeleo wa SADC 2020 – 2030; Agenda 2063 ya Umoja wa Afrika; na Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa 2030. Kwa Tanzania, dhana ya Uchumi wa Buluu unahusisha shughuli za kiuchumi na kijamii zinazotekelezwa katika bahari, maziwa, mito, mabwawa na maji chini ya ardhi bila kuathiri mazingira’. Tafsiri hii inaendana na tafsiri ya Umoja wa Afrika kwa kuwa imejumuisha maji bahari na baridi. Tanzania imekuwa ikitekeleza shughuli za Uchumi wa Buluu kupitia sekta mbalimbali zenye mnasaba na Uchumi wa Buluu ambazo ni pamoja na: Uvuvi; Maliasili na Utalii; Maji; Umwagiliaji; Nishati; Uchukuzi; Madini; Uwekezaji, Viwanda na Biashara; na Uhifadhi wa Mazingira. Uchumi wa Buluu una umuhimu mkubwa kwa Tanzania kutokana na wingi wa rasilimali zilizopo katika maji bahari na maji baridi. Rasilimali hizo zinajumuisha: Kilomita za mraba 61,500 za maeneo ya maji baridi yanayofaa kwa matumizi mbalimbali yanayokadiriwa kuwa na mita za ujazo bilioni 126 kwa mwaka. Aidha, Tanzania ina Kilomita za mraba 64,000 za maji ya kitaifa katika bahari; na Kilomita za mraba 223,000 za Ukanda Maalumu wa Uchumi wa Bahari. Vilevile, ina ukanda wa pwani ya bahari wenye urefu wa kilomita 1,424 ambao ni muhimu kwa shughuli za uvuvi, ukuzaji viumbe maji na utalii. Pia, ina eneo la hekta milioni 29.4 linalofaa kwa kilimo cha umwagiliaji. 1 Kuna misitu ya mwambao yenye ukubwa wa takribani kilomita za mraba 700; eneo la misitu ya mikoko kilomita za mraba 1,440; na mwamba wa matumbawe wenye ukubwa wa kilomita za mraba 3,580. Tanzania pia ina maeneo yaliyohifadhiwa kisheria yenye ukubwa wa kilomita za mraba 307,800 sawa na asilimia 32.5 ya eneo lote la nchi yanayojumuisha hifadhi zenye mnasaba na Uchumi wa Buluu. Kadhalika, kuna aina takribani 33 za samaki wa maji bahari na 17 za samaki wa maji baridi wanaoweza kuvunwa. Aidha, kuna futi za ujazo takribani Trilioni 47.13 za nishati ya gesi asilia baharini; na bandari rasmi 86 na zisizo rasmi 885 kwa ajili ya usafirishaji wa shehena za bidhaa mbalimbali. Vilevile, kuna madini katika bahari kuu yakijumuisha Nickel, Manganese, Cobalt Polymetallic Manganese Nodules, Polymetallic Manganese Sulphides na Cobalt-Rich Ferromanganese Crust. Hivyo, ili rasilimali hizi ziwe na manufaa zaidi kwa Taifa, Serikali imeamua kuzifungamanisha katika misingi ya Uchumi wa Buluu. Aidha, hitaji la uandaaji wa Sera ya Taifa ya Uchumi wa Buluu umetokana pia na changamoto zilizopo katika matumizi endelevu ya rasilimali za Uchumi wa Buluu. Changamoto hizo ni pamoja na: Kukosekana kwa mfumo jumuishi wa kitaasisi wa uratibu wa shughuli za Uchumi wa Buluu; Kukosekana kwa Mpango wa Matumizi wa Maeneo ya Maji; Kukosekana kwa uwekezaji wa kimkakati na fungamanishi katika matumizi ya rasilimali za Uchumi wa Buluu; Kukosekana kwa mfumo jumuishi wa kitaasisi wa usimamizi wa rasilimali za Uchumi wa Buluu katika eneo la Ukanda Maalumu wa Uchumi wa Bahari na Bahari kuu; na Uhaba wa utafiti na ujuzi katika matumizi ya rasilimali za Uchumi wa Buluu.

  56. 1.1. HALI ILIVYO Shughuli za Uchumi wa Buluu hapa nchini zinatekelezwa na Sekta za: Uvuvi, Nishati, Uchukuzi, Maliasili na Utalii, Maji, Umwagiliaji, Madini, Uhifadhi wa Mazingira, Uwekezaji, Viwanda na Biashara. Serikali imeweka nyenzo mbalimbali za Kisera na Kisheria ambapo pamoja na mambo mengine zimeweka utaratibu wa usimamizi na uratibu wa shughuli za Uchumi wa Buluu katika sekta husika. Kwa upande wa Tanzania Bara, Sera za sekta zinazosimamia shughuli za Uchumi wa Buluu ni pamoja na: Sera ya Taifa ya Uvuvi (2015); Sera ya Taifa ya Nishati (2015); Sera ya Taifa ya Usafirishaji (2003); Sera ya Taifa ya Utalii (1999); Sera ya Taifa ya Maji (2002); Sera ya Taifa ya Umwagiliaji (2010); Sera ya Taifa ya Madini (2009); Sera ya Maendeleo Endelevu ya Viwanda (1996 – 2020); Sera ya Taifa ya Kilimo (2013); Sera ya Taifa ya Biashara (2003); Sera ya Uwekezaji (1996); Sera ya Maendeleo ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo (2003); Sera ya Taifa ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (2004); Sera ya Malikale (2008); Sera ya Taifa ya Misitu (1998); Sera ya Masoko ya Mazao na Bidhaa za Kilimo (2008); Sera ya Taifa ya Jinsia na Maendeleo ya Wanawake (2023); na Sera ya Taifa ya Mazingira (2021). 2 Aidha, Sheria zinazotekelezwa na sekta hizo zinajumuisha: Sheria ya Uvuvi, Sura 279; Sheria ya Usimamizi na Uendelezaji wa Uvuvi wa Bahari Kuu, Sura 388; Sheria ya Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu, Sura 146; Sheria ya Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi, Sura 280; Sheria ya Petroli, Sura 392; Sheria ya Umeme, Sura 131; Sheria ya Nishati Vijijini, Sura 321; Sheria ya Usimamizi wa Mapato ya Mafuta na Gesi, Sura 328; Sheria ya Usafirishaji Majini, Sura 165; Sheria ya Uwakala wa Meli Tanzania, Sura 415; Sheria ya Bandari, Sura 166; Sheria ya Chuo cha Bahari Dar es Salaam, Sura 253; Sheria ya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji, Sura 187; Sheria ya Utalii, Sura 65; Sheria ya Usimamizi wa Rasilimali za Maji, Sura 331; Sheria ya Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira, Sura 272; Sheria ya Taifa ya Umwagiliaji, Sura 435; Sheria ya Malikale, Sura 550; Sheria ya Uwekezaji, Sura 38; Sheria ya Madini, Sura 123; Sheria ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, Sura 157; Sheria ya Mamlaka ya Nchi Kuhusiana na Umiliki wa Maliasili, Sura 449; Sheria ya Mamlaka ya Nchi kuhusu Utajiri na Maliasili za Nchi (Mapitio na Majadiliano Kuhusu Masharti Hasi), Sura 450; na Sheria ya Usimamizi wa Mazingira, Sura 191. Kwa mwaka 2023, mafanikio mbalimbali yaliyopatikana kupitia utekelezaji wa sera na sheria za sekta zenye mnasaba wa Uchumi wa Buluu ni pamoja na: Kuzalisha tani 513,802.47 za mazao ya uvuvi yenye thamani ya Shilingi trilioni 3.5. Mazao hayo yanajumuisha tani 479,976.62 kutoka uvuvi wa maji ya asili (uvuvi katika maji baridi ukichangia asilimia 85 na maji bahari asilimia 15) na tani 33,825.85 kutoka ukuzaji viumbe maji zinazojumuisha ufugaji wa samaki, kilimo cha mwani, nyasi bahari na ufugaji wa matango bahari; Kugunduliwa kwa gesi asilia takribani futi za ujazo trilioni

  57. 57.54. Kati ya hizo, futi za ujazo trilioni 47.13 zinapatikana kwenye kina kirefu cha Bahari ya Hindi; Kuongezeka kwa idadi ya meli za kitalii kufikia meli nane (8) zilizosafirisha jumla ya watalii 965 kutoka nchi mbalimbali kuja nchini. Mafanikio mengine ni pamoja na: Kuimarika kwa hali ya upatikanaji wa huduma ya maji vijijini kutoka wastani wa asilimia 58 mwaka 2018 na kufikia wastani wa asilimia 77 mwaka 2023; Kuimarika kwa hali ya upatikanaji wa huduma ya maji mijini kutoka wastani wa asilimia 78 mwaka 2018 na kufikia asilimia 88 mwaka 2023; Kuongezeka kwa uzalishaji wa zao la mpunga kutoka tani 714,000 mwaka 1990 hadi kufikia tani 3,587,981.54 mwaka 2023; na Kuongezeka kwa shehena ya mizigo iliyohudumiwa katika bandari nchini kutoka tani 13,727,770 za mizigo mwaka 2012/2013 hadi kufikia tani 24,899,000 za mizigo mwaka 2022/23 sawa na ongezeko la asilimia 81. Fursa zilizopo katika rasilimali za Uchumi wa Buluu ni pamoja na: Uwekezaji katika miundombinu ya utafutaji, uchimbaji na uzalishaji wa nishati katika maeneo ya maji; Uwepo wa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi wenye nia ya kuwekeza kwenye rasilimali maji; Uwepo wa masoko ndani na nje ya nchi kwa mazao yanayopatikana kwenye maji kama vile mafuta, gesi na samaki; Kuongeza wigo wa utekelezaji wa shughuli za kiuchumi katika Ukanda Maalumu wa Bahari na Bahari Kuu; Kuongeza 3 uzalishaji wa mazao kupitia kilimo cha umwagiliaji; na uwekezaji katika tafiti na teknolojia mbalimbali kwa ajili ya kukuza na kuendeleza shughuli za Uchumi wa Buluu nchini. Pamoja na uwepo wa miongozo ya kisera na kisheria inayosimamia na kuratibu utekelezaji wa shughuli za Uchumi wa Buluu, fursa za Uchumi wa Buluu zilizopo nchini hazijatumika ipasavyo kutokana na changamoto mtambuka ambazo haziwezi kutatuliwa na sekta moja. Changamoto hizo ni pamoja na: Kukosekana kwa mfumo jumuishi wa kitaasisi wa uratibu wa shughuli za Uchumi wa Buluu; Kukosekana kwa Mpango wa Matumizi wa Maeneo ya Maji; Uwekezaji usio wa kimkakati na fungamanishi katika matumizi ya rasilimali za Uchumi wa Buluu; na Uhaba wa utafiti na ujuzi katika matumizi ya rasilimali za Uchumi wa Buluu. Hali halisi ya kila changamoto iliyoainishwa imefafanuliwa katika kipengele 1.1.1 hadi 1.1.5.

  58. 1.1.1 Uratibu wa shughuli za Uchumi wa Buluu Utekelezaji wa shughuli za Uchumi wa Buluu kupitia sekta moja moja haujawa na tija kutokana na kukosekana kwa uratibu jumuishi. Hali hii, inachangia kuwepo kwa uwekezaji usiofungamanishi unaosababisha uwekezaji wa sekta moja kutonufaisha sekta nyingine; Matumizi yasiyoendelevu ya maeneo ya bahari, mito, maziwa, mabwawa, na maeneo oevu ambayo yanachangia upotevu wa rasilimali za maji na migongano baina ya watumiaji wa rasilimali hizo. Mathalani, migongano kati ya Sekta ya Usafirishaji kwa njia ya maji na Sekta ya Nishati katika utekelezaji wa baadhi ya majukumu kama kuainisha na kutambua njia za meli baharini na kufanya shughuli za utafutaji na uendelezaji wa gesi asilia na mafuta; na Uwepo wa shughuli moja kugharamiwa na Sekta mbalimbali bila uwepo wa utaratibu maalumu. Vilevile, kuendelea kuongezeka kwa makosa ya jinai kwenye maeneo na matumizi ya rasilimali za maji ikiwemo uvuvi na biashara haramu ya mazao ya uvuvi (vilipuzi baharini na kemikali kwenye maziwa na mito); uharamia kupitia utekaji wa meli na uporaji wavuvi; magendo kupitia bandari bubu zinazokadiriwa kufika 885; uhalifu wa mitandao unaohusisha kuingilia mawasiliano ya meli; uchafuzi wa mazingira ya bahari na maziwa kutokana na taka za plastiki, umwagaji wa mafuta na taka kutoka melini, utiririshaji wa majitaka, utiririshaji wa kemikali kutoka viwandani na viuatilifu vya kilimo; usafirishaji haramu wa binadamu; usafirishaji wa dawa za kulevya; na uvunaji na usafirishaji haramu wa mazao ya misitu ya mikoko. Ili Tanzania iweze kunufaika ipasavyo na fursa zitokanazo na shughuli za Uchumi wa Buluu kuna uhitaji wa kuwa na uratibu jumuishi wa shughuli za Uchumi wa Buluu ambao utaweka mfumo wa uratibu miongoni mwa wadau mbalimbali wanaosimamia na kutekeleza shughuli za Uchumi wa Buluu hapa nchini. 4

  59. 1.1.2 Matumizi ya Maeneo ya Maji Uwepo wa rasilimali maji kunawezesha utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Uchumi wa Buluu ikiwemo uvuvi, ukuzaji viumbe maji, utalii wa fukwe, nishati, uchukuzi, madini na kilimo cha umwagiliaji. Pamoja na wizara za kisekta kutekeleza sera na kusimamia sheria katika matumizi ya rasilimali maji, mahitaji ya matumizi yanazidi kuongeza kwa kasi kutokana na ongezeko la watu na kupanuka kwa shughuli za kiuchumi zinazohitaji rasilimali maji. Kutokana na ongezeko hilo, kumeibuka migongano kati ya watumiaji mbalimbali wa rasilimali hizo. Mfano, migongano kati ya wavuvi na wakulima wa mwani; wachimbaji wadogo wa chumvi na wahifadhi wa misitu ya mikoko; na wakulima, wafugaji na wahifadhi wa vyanzo vya maji ambayo inaweza kuathiri miradi mikubwa ya kimkakati inayotekelezwa nchini. Ukuaji wa Uchumi wa Buluu unatarajiwa kuongeza shughuli ambazo zitakuwa na ushindani na ukinzani katika matumizi ya maeneo yamaji kama vile utafutaji na uchimbaji wa mafuta, gesi asilia na madini chini ya maji, uzalishaji wa nishati kwa kutumia mawimbi au upepo, usafirishaji wa meli na ukuzaji viumbe maji. Iwapo hakutakuwa na utaratibu maalumu wa kupanga matumizi ya maeneo yamaji kwa shughuli hizo, inaweza kuleta migogoro na uharibifu wa mazingira na hivyo kuhatarisha uendelevu wa shughuli za Uchumi wa Buluu nchini. Hivyo, upo umuhimu wa kuwa na Mpango wa Matumizi wa Maeneo ya Maji ili kuwezesha Nchi kunufaika ipasavyo na fursa za Uchumi wa Buluu. Msingi mkuu wa mpango huu ni kupanga matumizi ya maeneo ya maji kwa kuzingatia mahitaji ya shughuli za kiuchumi, kijamii na uhifadhi wa mifumo ikolojia na mazingira.

  60. 1.1.3 Usimamizi katika eneo la Ukanda Maalumu wa Uchumi wa Bahari na Bahari Kuu Umoja wa Mataifa ulipitisha Mkataba wa Sheria ya Bahari mwaka 1982 ambao pamoja na mambo mengine ulielekeza nchi wanachama kutenga eneo la Ukanda Maalumu wa Uchumi wa Bahari lenye upana wa maili za bahari zisizozidi 200. Lengo kuu la Mkataba huo ni kusimamia na kuziwezesha nchi wanachama kunufaika ipasavyo na rasilimali za bahari kama vile: Utafutaji na uchimbaji wa nishati ya mafuta na gesi asilia; Ufuaji wa nishati ya umeme kwa njia ya mawimbi, mikondo ya maji na upepo; na Utafutaji na uchimbaji wa madini na Uvuvi. Tanzania iliridhia Mkataba huo mwaka 1985 na mwaka 1989 ikatunga Sheria ya Bahari ya Kitaifa na Ukanda Maalumu wa Uchumi wa Bahari, Sura 238 inayoainisha eneo la maji ya ndani na maji ya kitaifa kwa upana wa maili za bahari 12 na eneo la Ukanda Maalumu wa Uchumi wa Bahari wenye upana wa maili za bahari 200. Kwa ujumla eneo la Ukanda Maalumu wa Uchumi wa Bahari ya Tanzania lina ukubwa wa kilomita za mraba 223,000. 5 Ili kunufaika na fursa zilizopo katika eneo la Ukanda Maalumu wa Uchumi wa Bahari na Bahari Kuu, Tanzania ilitunga Sheria ya Usimamizi na Uendelezaji wa Uvuvi wa Bahari Kuu, Sura 388 iliyoanzisha Mamlaka ya Kusimamia Uvuvi wa Bahari Kuu ambayo ni Taasisi ya Muungano. Hata hivyo, rasilimali nyingine zilizopo katika eneo la Ukanda Maalumu wa Uchumi wa Bahari na Bahari Kuu kama vile mafuta na gesi asilia, na madini hazijatambuliwa na sheria hiyo. Hali hiyo inasababisha nchi kutokunufaika ipasavyo na rasilimali hizo. Kwa muktadha huo, ipo haja ya kupitia upya Sheria ya Usimamizi na Uendelezaji wa Uvuvi wa Bahari Kuu, Sura 388 kwa lengo la kuiongezea majukumu ya Taasisi hiyo ili kuiwezesha kuratibu shughuli za Uchumi wa Buluu zaidi ya uvuvi katika Ukanda Maalumu wa Uchumi wa Bahari na Bahari Kuu.

  61. 1.1.4 Uwekezaji Uwekezaji unaofanyika nchini katika sekta za Uchumi wa Buluu umekuwa ukilenga sekta moja moja usiojumuishi na hivyo kuwa na tija ndogo. Aidha, miundombinu na teknolojia duni zinazotumika kwenye uwekezaji wa viwanda vilivyopo nchini inasababisha bidhaa zinazozalishwa kutokukidhi viwango na mahitaji ya soko la ndani na nje ya nchi hivyo kupelekea kukosa ushindani. Hali hii imechangia uwekezaji kutokufanyika ipasavyo kwenye baadhi ya shughuli za Uchumi wa Buluu ikiwemo uvuvi, uchimbaji wa madini, mafuta, na uzalishaji wa umeme. Ili kuongeza tija ya uwekezaji unaofanyika ni muhimu kubaini maeneo yanayohitaji uwekezaji wa kimkakati ambao unafungamanisha zaidi ya sekta moja ya Uchumi wa Buluu. Uwekezaji huo huleta matokeo makubwa ikiwemo kupata thamani ya fedha inayowekezwa. Mathalani, uwekezaji katika bandari ya uvuvi unaweza kufungamanishwa na viwanda vya uchakataji, miundombinu ya kuhifadhia samaki, soko la samaki, utalii wa meli na migahawa ya mazao ya uvuvi na hivyo kuwa na manufaa makubwa zaidi kwa Uchumi wa Buluu. Pamoja na uwekezaji wa Serikali katika miundombinu na huduma mbalimbali, bado kuna umuhimu wa kujenga uelewa wa fursa zilizopo na kuweka vivutio stahiki ili kuhamasisha uwekezaji wa sekta binafsi. Aidha, ili kuongeza wigo wa uwekezaji, Serikali kwa kushirikiana na wadau wengine itatumia fursa zilizopo kupata mitaji kama vile Hati Fungani za Buluu na kutumia rasilimali za Uchumi wa Buluu kupitia Biashara ya Kaboni. Aidha, ili kunufaika na rasilimali za Uchumi wa Buluu uwekezaji unapaswa kufanyika katika viwanda vya uchakataji na uongezaji thamani bidhaa zitokanazo na rasilimali hizo kwa kuzingatia viwango vya ubora na ithibati kimataifa ili bidhaa zinazozalishwa ziwe shindani kimataifa na kuongeza upatikanaji wa fedha za kigeni. Hatua hii pia itazalisha ajira na kuongeza kipato kwa wadau mbalimbali katika mnyororo wa thamani wa rasilimali za Uchumi wa Buluu. 6

  62. 1.1.5 Utafiti katika Rasilimali za Sekta za Uchumi wa Buluu Utafiti katika rasilimali za sekta za Uchumi wa Buluu ni suala muhimu linalowezesha nchi kunufaika na fursa zilizopo. Katika sekta hizo, kumekuwa na tafiti mbalimbali kuhusu wingi na mtawanyiko wa rasilimali za Uchumi wa Buluu. Hata hivyo, tafiti hizo zinakosa taarifa toshelevu zinazowezesha fursa za Uchumi wa Buluu kutumika ipasavyo katika maendeleo ya taifa na ustawi wa jamii kwa ujumla. Upungufu huo unatokana na changamoto mbalimbali zikiwemo uhaba wa wataalamu, uhaulishaji na uelewa mdogo wa teknolojia mpya na zinazoibukia kuhusu rasilimali za Uchumi wa Buluu. Aidha, upo uhaba wa miundombinu na teknolojia za kisasa katika kufanya tafiti na ukusanyaji wa taarifa na takwimu, mfano ukosefu wa maabara zenye ithibati na teknoloija za kutafiti rasilimali zilipo katika sakafu ya bahari, mifumo ikolojia ya maji, na nishati jadidifu kutokana na upepo wa baharini. Changamoto nyingine ni pamoja na: utengamano mdogo katika kufanya utafiti baina ya sekta moja na nyingine; usambazaji mdogo wa matokeo ya utafiti na teknolojia ili ziweze kutumika katika jamii; ushiriki mdogo wa sekta binafsi katika shughuli za utafiti; na mahitaji makubwa ya rasilimali fedha kwa ajili ya kugharamia utafiti. Hali hii inasababisha kutokuwa na takwimu sahihi na kutotambua faida ya matumizi ya rasilimali za Uchumi wa Buluu. Kwa muktadha huo, kuna haja ya kuimarisha utafiti katika matumizi ya rasilimali za Uchumi wa Buluu. 7 SURA YA PILI

  63. 2.0 UMUHIMU WA SERA, DIRA, DHIMA NA MALENGO YA SERA

  64. 2.1. Umuhimu wa Sera Tanzania ina fursa ya kunufaika kiuchumi na kijamii kutokana na matumizi endelevu ya rasilimali za Uchumi wa Buluu kulingana na wingi wa rasilimali hizo. Shughuli za Uchumi wa Buluu kwa kiasi kikubwa zimekuwa zikitekelezwa na sekta zenye mnasaba na Uchumi wa Buluu kupitia sera na sheria za sekta husika. Pamoja na uwepo wa sera na sheria hizo, kumekuwepo na changamoto mtambuka zinazochangia Taifa kutonufaika ipasavyo na rasilimali zitokanazo na shughuli za Uchumi wa Buluu ambazo zinajumuisha: Kukosekana kwa mfumo jumuishi wa kitaasisi wa uratibu wa shughuli za Uchumi wa Buluu; Kukosekana kwa Mpango wa Matumizi wa Maeneo ya Maji; Uwekezaji usio wa kimkakati na fungamanishi katika matumizi ya rasilimali za Uchumi wa Buluu; na Uhaba wa utafiti na ujuzi katika matumizi ya rasilimali za Uchumi wa Buluu. Changamoto hizo zimesababisha athari mbalimbali katika utekelezaji wa shughuli za Uchumi wa Buluu zikiwemo: Kuwepo kwa migongano katika utekelezaji wa majukumu na matumizi ya maeneo ya maji miongoni mwa wadau mbalimbali; kuwepo kwa uwekezaji ambao siyo jumuishi na fungamanishi; Uwepo wa shughuli moja kugharamiwa na sekta mbalimbali bila uwepo wa utaratibu maalumu; na Kukosekana kwa takwimu sahihi pamoja na uwezo mdogo wa kitaasisi katika kufanya tafiti za uendelezaji wa rasilimali za Uchumi wa Buluu. Sera ya Taifa ya Uchumi wa Buluu ni nyenzo muhimu ya kuwezesha nchi kunufaika na fursa zitokanazo na rasilimali za Uchumi wa Buluu ili kukuza uchumi wa Taifa kwa maendeleo endelevu. Sera hii haikusudii kuondoa sera, majukumu, sheria, mikakati ya sekta nyingine zenye mnasaba na Uchumi wa Buluu bali inakusudia kuweka uratibu jumuishi ili kuongeza mchango wa sekta za Uchumi wa Buluu katika Pato la Taifa na hivyo kukuza uchumi na kuwa na maendeleo endelevu.

  65. 2.2. Dira, Dhima na Malengo ya Sera

  66. 2.2.1. Dira Tanzania yenye Uchumi wa Buluu imara, endelevu na jumuishi.

  67. 2.2.2. Dhima Kuwezesha usimamizi madhubuti na matumizi endelevu ya rasilimali za Uchumi wa Buluu. 8

  68. 2.2.3. Malengo ya Sera

  69. 2.2.3.1. Lengo Kuu Kutumia rasilimali za Uchumi wa Buluu ili kukuza uchumi wa Taifa kwa maendeleo endelevu.

  70. 2.2.3.2. Malengo Mahsusi Malengo mahsusi ya Sera ni: i) Kuimarisha uratibu wa shughuli za Uchumi wa Buluu; ii) Kuhamasisha matumizi ya maeneo ya maji; iii) Kuhamasisha uwekezaji wa kimkakati na fungamanishi katika matumizi ya rasilimali za Uchumi wa Buluu; iv) Kuimarisha utafiti katika matumizi ya rasilimali za Uchumi wa Buluu; na v) Kuhamasisha uzingatiaji wa masuala mtambuka katika utekelezaji wa shughuli za Uchumi wa Buluu. 9 SURA YA TATU

  71. 3.0 HOJA NA MATAMKO YA SERA Sehemu hii inaainisha masuala mahsusi yatakayozingatiwa na Sera. Masuala hayo ni: Uratibu wa masuala ya Uchumi wa Buluu; Matumizi ya maeneo ya maji; Uwekezaji; na Utafiti kuhusu uendelezaji wa rasilimali za Uchumi wa Buluu.

  72. 3.1. Uratibu wa masuala ya Uchumi wa Buluu Utekelezaji wa shughuli za Uchumi wa Buluu kupitia sekta moja moja haujawa na tija kutokana na kukosekana kwa uratibu jumuishi unaosababishwa na mawasiliano hafifu miongoni mwa wadau wa shughuli za Uchumi wa Buluu. Hali hii, inasababisha kuwepo kwa uwekezaji usiofungamanishi unaopelekea uwekezaji wa sekta moja kutonufaisha sekta nyingine; utekelezaji wa miradi mbalimbali usiofungamanishi unaosababisha upotevu wa fedha; kuendelea kuongezeka kwa makosa ya jinai kwenye maeneo na matumizi ya rasilimali za maji; matumizi yasiyoendelevu ya rasilimali za maji. Aidha, baadhi za shughuli za uchumi buluu kama utafutaji wa nishati na gesi asilia, ufuaji wa nishati ya umeme kwa njia mawimbi, mikondo ya maji na upepo; utafutaji na uchimbaji wa madini zinazofanyika katika bahari kuu zinakosa mfumo wa pamoja wa uratibu na usimamizi kwa pande zote mbili za muungano. Kwa muktadha huu, kuna umuhimu wa kuwa na mfumo jumuishi wa kitaasisi wa uratibu wa Serikali na wadau wengine katika utekelezaji na usimamizi wa shughuli za Uchumi wa Buluu na kuweka mfumo wa kisheria ili shughuli zote zinazofanyika katika maeneo ya maji ikiwemo Ukanda Maalumu wa Uchumi wa Bahari na Bahari Kuu ziweze kuratibiwa na kusimamiwa ipasavyo. Lengo Kuimarisha uratibu wa shughuli za Uchumi wa Buluu. Matamko ya Sera Serikali kwa kushirikiana na wadau wengine itafanya yafuatayo: i) Kuweka mfumo jumuishi wa kitaasisi wa uratibu wa shughuli za Uchumi wa Buluu; ii) Kuimarisha uratibu wa rasilimali za Uchumi wa Buluu katika eneo la Ukanda Maalumu wa Uchumi wa Bahari na Bahari Kuu; na iii) Kuimarisha usimamizi wa rasilimali za Uchumi wa Buluu katika maeneo ya maji. 10

  73. 3.2. Matumizi ya maeneo ya maji Uwepo wa rasilimali maji katika bahari na maji baridi kunawezesha utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Uchumi wa Buluu ikiwemo uvuvi, ukuzaji viumbe maji, utalii wa fukwe, nishati, uchukuzi, madini na kilimo cha umwagiliaji. Mahitaji ya rasilimali maji katika shughuli hizo yanazidi kuongezeka kwa kasi kutokana na ongezeko la watu na kupanuka kwa shughuli za kiuchumi. Hali hii inasababisha migongano kati ya watumiaji wa rasilimali hizo. Vilevile, ukuaji wa shughuli za Uchumi wa Buluu unatarajia kuongeza ushindani na ukinzani katika matumizi ya rasilimali maji kama vile utafutaji na uchimbaji wa mafuta, gesi asilia na madini chini ya sakafu ya Bahari; uzalishaji wa nishati ya umeme kwa kutumia mawimbi au upepo; usafirishaji; uvuvi na ukuzaji viumbe maji. Hivyo, upo umuhimu wa kuwa na mpango wa matumizi bora ya maeneo ya maji ambao utatoa fursa kwa shughuli zote za kiuchumi kufanyika kwa uendelevu bila migongano au kuathiri mazingira ya sasa na ya baadaye. Lengo Kuhamasisha matumizi endelevu ya rasilimali za maji. Tamko la Sera Serikali kwa kushirikiana na wadau wengine itafanya yafuatayo: i) Kuimarisha matumizi ya maeneo ya maji; na ii) Kujenga uelewa wa jamii kuhusu matumizi endelevu ya rasilimali za Uchumi wa Buluu.

  74. 3.3. Uwekezaji Uwekezaji unaofanyika nchini katika sekta za Uchumi wa Buluu umekuwa ukilenga sekta moja moja usiojumuishi na hivyo kuwa na tija ndogo. Aidha, miundombinu na teknolojia duni zinazotumika kwenye uwekezaji wa viwanda vilivyopo nchini inasababisha bidhaa zinazozalishwa kutokukidhi viwango na mahitaji ya soko la ndani na nje ya nchi hivyo kupelekea kukosa ushindani. Hali hii imechangia uwekezaji kutokufanyika ipasavyo kwenye baadhi ya shughuli za Uchumi wa Buluu ikiwemo uvuvi, uchimbaji wa madini, mafuta, na uzalishaji wa umeme. Ili kuongeza tija ya uwekezaji unaofanyika, ni muhimu kubaini maeneo yanayohitaji uwekezaji wa kimkakati ambao unafungamanisha zaidi ya sekta moja ya Uchumi wa Buluu. Vilevile, kuna uwekezaji mdogo katika viwanda vya uchakataji na uongezaji thamani bidhaa zitokanazo na rasilimali ili kuongeza ajira na kipato kwa wadau mbalimbali katika mnyororo wa thamani wa mazao ya Uchumi wa Buluu. Kadhalika, shughuli zinazofanyika katika rasilimali za Uchumi wa Buluu kutokidhi viwango vya ubora na 11 ithibati kimataifa vitakavyowezesha bidhaa za Tanzania ziwe shindani katika soko la dunia ambapo mauzo yake yataongeza upatikanaji wa fedha za kigeni. Lengo Kuhamasisha uwekezaji wa kimkakati na fungamanishi katika matumizi ya rasilimali za Uchumi wa Buluu. Tamko la Sera Serikali kwa kushirikiana na wadau wengine itafanya yafuatayo: i) Kuhamasisha uwekezaji jumuishi unaofungamanisha zaidi ya sekta moja za Uchumi wa Buluu; ii) Kuhamasisha ushiriki wa sekta binafsi katika shughuli za uwekezaji za Uchumi wa Buluu; na iii) Kuhamasisha uwekezaji katika uongezaji thamani wa bidhaa zitokanazo na rasilimali za Uchumi wa Buluu.

  75. 3.4. Utafiti katika Rasilimali za Sekta za Uchumi wa Buluu Utafiti una mchango mkubwa katika kuendeleza na kuwezesha Tanzania kunufaika na fursa zilizopo katika rasilimali za Uchumi wa Buluu. Utafiti pia unawezesha Serikali kuweka mikakati na mipango sahihi ya uendelezaji na usimamizi wa shughuli za uchumi nchini. Hata hivyo, Tanzania inakabiliwa na changamoto ya uwezo mdogo wa kufanya utafiti kuhusu rasilimali za Uchumi wa Buluu hususani katika maeneo ya utambuzi, uzalishaji na matumizi. Hali hii inachangiwa na uhaba wa miundombinu na teknolojia za kisasa katika kufanya tafiti hususani maabara za kisasa na teknoloija za kutafiti rasilimali zilipo, uwepo wa wataalamu wachache katika kufanya tafiti za rasilimali za Uchumi wa Buluu, ikiwa ni pamoja na wanasayansi wa baiolojia za kwenye maji, hali ya hewa na mabadiliko ya tabianchi na wataalamu wenye ujuzi na uelewa katika tasnia ya uchukuzi kwenye maji. Aidha, changamoto nyingine ni pamoja na utengamano mdogo katika kufanya utafiti ambapo utafiti hufanyika katika sekta moja bila kushirikisha sekta nyingine zenye mnasaba wa Uchumi wa Buluu; uhaulishaji mdogo wa tafiti na teknolojia ili kutumika kwa jamii; ushiriki mdogo wa sekta binafsi katika shughuli za utafiti; na upungufu wa rasilimali fedha kwa ajili ya kugharamia shughuli za utafiti. Lengo Kuimarisha utafiti katika matumizi ya rasilimali za Uchumi wa Buluu. Tamko la Sera Serikali kwa kushirikiana na wadau wengine itafanya yafuatayo: 12 i) Kuhamasisha utafiti jumuishi unaoshirikisha sekta nyingine zenye mnasaba na Uchumi wa Buluu; ii) Kuhakikisha uwepo miundombinu bora na teknolojia za kisasa katika taasisi za utafiti wa rasilimali za Uchumi wa Buluu; iii) kuhakikisha uwepo wa watafiti wa kutosha wenye ujuzi sahihi katika kuendeleza utafiti wa rasilimali za Uchumi wa Buluu; iv) kuhakikisha matokeo ya utafiti, teknolojia na ujuzi zinawafikia wadau wote wa Uchumi wa Buluu; na v) Kuhamasisha ushiriki wa sekta binafsi katika shughuli za utafiti.

  76. 3.5. Masuala Mtambuka

  77. 3.5.1. Jinsia Masuala ya jinsia ni muhimu kuzingatiwa katika usimamizi wa rasilimali za Uchumi wa Buluu. Kwa kutambua umuhimu wa masuala ya jinsia, Serikali imeandaa, kusimamia na kutekeleza sera, sheria, mikakati na miongozo mbalimbali inayohimiza uzingatiaji wa masuala ya jinsia katika usimamizi na utekelezaji wa shughuli za Uchumi wa Buluu. Pamoja na jitihada hizo, ushirikishaji na uwezeshaji wanawake kiuchumi unahitaji kuimarishwa katika usimamizi na uendelezaji wa rasilimali za Uchumi wa Buluu. Lengo Kuhamasisha usawa katika ushiriki wa wanaume na wanawake kwenye shughuli zenye mnasaba na Uchumi wa Buluu. Tamko la Sera Serikali kwa kushirikiana na wadau wengine itafanya yafuatayo: i) Kuhakikisha uzingatiaji wa masuala ya jinsia katika sera, mikakati na mipango ya uendelezaji wa rasilimali za Uchumi wa Buluu kwa sekta zenye mnasaba na Uchumi wa Buluu; na ii) Kuhakikisha usawa wa jinsia katika kutumia fursa za Uchumi wa Buluu. 13

  78. 3.5.2. Utawala Bora Utawala Bora ni moja ya misingi muhimu ya usimamizi wa rasilimali nchini ambao umeingizwa katika sera, mikakati, mipango na programu mbalimbali. Serikali na wadau wana jukumu la kuhakikisha misingi ya utawala bora inajumuishwa katika jitihada za hifadhi ya rasilimali za Uchumi wa Buluu. Aidha, usimamizi madhubuti wa sheria za usimamizi wa rasilimali hizo ni muhimu katika kuhakikisha uwazi, uwajibikaji na ushirikishwaji unazingatiwa ili kutoa motisha kwa jamii kushiriki kikamilifu katika shughuli za Uchumi wa Buluu nchini. Lengo Kuhamasisha utawala bora katika usimamizi wa rasilimali za Uchumi wa Buluu. Tamko la Sera Serikali itaimarisha uzingatiaji wa masuala ya utawala bora katika usimamizi wa rasilimali za Uchumi wa Buluu. 14 SURA YA NNE

  79. 4.0 MUUNDO WA KISHERIA Sera ya Taifa ya Uchumi wa Buluu itatekelezwa kwa kuzingatia mfumo wa kisheria uliopo kwenye sekta zinazotekeleza shughuli zenye mnasaba na Uchumi wa Buluu. Aidha, sera na sheria za kisekta ndizo zitakuwa msingi wa utekelezaji wa masuala ya Uchumi wa Buluu. Hata hivyo, kwa kuzingatia changamoto ya kukosekana kwa mfumo jumuishi wa uratibu wa shughuli za Uchumi wa Buluu katika eneo la Ukanda Maalumu wa Uchumi wa Bahari na Bahari Kuu, Sheria ya Usimamizi na Uendelezaji wa Uvuvi wa Bahari Kuu, Sura 388 itafanyiwa marekebisho ili kubadilisha jina la “Mamlaka ya Kusimamia Uvuvi wa Bahari Kuu” kuwa “Mamlaka ya Usimamizi wa Bahari Kuu” kuiwezesha taasisi hii kuratibu matumizi ya rasilimali zote za Uchumi wa Buluu zilizopo katika eneo la Ukanda Maalumu wa Uchumi wa Bahari na Bahari Kuu. Aidha, ili kuendana na mahitaji ya Sera ya Taifa ya Uchumi wa Buluu ikiwemo kuboresha utekelezaji katika sekta, wizara za kisekta zinaweza kufanya mapitio ya sheria zake na kuzifanyia marekebisho pale itakapohitajika au kutungwa kwa sheria mpya. 15 SURA YA TANO

  80. 5.0 MUUNDO WA KITAASISI Sera ya Taifa ya Uchumi wa Buluu itatekelezwa kwa ushirikiano baina ya wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na Sekta za Umma, Sekta Binafsi, Jumuiya za Kikanda, Kimataifa na Wadau wengine wa Maendeleo. Utekelezaji wa Sera hii utafanywa katika ngazi za wizara za kisekta zinazotekeleza shughuli zenye mnasaba na Uchumi wa Buluu chini ya uratibu wa Ofisi yenye dhamana na uratibu wa Uchumi wa Buluu.

  81. 5.1. Majukumu na Wajibu wa Wadau Majukumu yatakayotekelezwa na wadau kuanzia ngazi ya uratibu, usimamizi na utekelezaji ni kama ifuatavyo:

  82. 5.1.1. Ofisi yenye dhamana ya uratibu wa Uchumi wa Buluu Ofisi hii itakuwa na majukumu yafuatayo: i) Kusimamia na kuratibu utekelezaji wa sera, mkakati, mipango na programu za Uchumi wa Buluu; ii) Kuratibu uaandaji na utekelezaji wa Mpango wa Matumizi ya Maeneo ya Maji; iii) Kutoa taarifa ya utekelezaji wa sera, mkakati, mipango na programu za Uchumi wa Buluu kwa Kamati ya Kitaifa ya Mawaziri; na iv) Kuwa Sekretarieti ya Kamati ya Kitaifa ya Mawaziri na Kamati ya Makatibu Wakuu inayoshughulikia shughuli za Uchumi wa Buluu.

  83. 5.1.2. Ofisi yenye dhamana ya Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa Kuratibu na kufuatilia utekelezaji wa Sera ya Uchumi wa Buluu kwenye Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa.

  84. 5.1.3. Ofisi yenye dhamana ya Mazingira na Muungano i) Kuandaa na kusimamia miongozo ya uhifadhi wa mazingira katika utekelezaji wa shughuli za uchumi wa buluu; na ii) Kuratibu masuala ya muungano katika utekelezaji wa shughuli za Uchumi wa Buluu.

  85. 5.1.4. Ofisi yenye dhamana ya Menejimenti ya Utumishi wa Umma Utawala Bora i) Kuratibu, kusimamia na kutoa miongozo ya masuala ya utawala bora katika utekelezaji wa shughuli za Uchumi wa Buluu; ii) Kuratibu uwanzishwaji wa Ofisi ya Uratibu wa shughuli za Uchumi wa Buluu; na 16 iii) Kuratibu uanzishwaji wa Taasisi ya Kuratibu na Kusimamia rasilimali zote za Uchumi wa Buluu zilizopo katika eneo la Ukanda Maalumu wa Uchumi wa Bahari na Bahari Kuu.

  86. 5.1.5. Ofisi yenye dhamana ya Mipango na Uwekezaji i) Kuhakikisha kuwa shughuli za Uchumi wa Buluu zimepewa kipaumbele katika mipango na mikakati ya maendeleo ya Taifa; ii) Kuweka mfumo wa tathmini ya mchango wa Uchumi wa Buluu katika Pato la Taifa; na iii) Kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji katika shughuli za Uchumi wa Buluu.

  87. 5.1.6. Ofisi yenye dhamana ya Uratibu wa shughuli za Serikali Kutoa mwongozo na kusimamia utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Uchumi wa Buluu.

  88. 5.1.7. Wizara yenye dhamana ya Fedha i) Kuhakikisha kuwa Wizara za Kisekta zinatenga fedha katika mipango na bajeti kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za Uchumi wa Buluu; ii) Kuratibu upatikanaji wa rasilimali fedha kutoka katika vyanzo bunifu na vyenye gharama nafuu ikijumuisha ubia kati ya sekta ya umma na binafsi; na iii) Kuwezesha upatikanaji wa mitaji kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za Uchumi wa Buluu.

  89. 5.1.8. Wizara za Kisekta

  90. 5.1.8.1. Wizara yenye dhamana ya Uvuvi i) Kusimamia uhifadhi na matumizi endelevu ya rasilimali za uvuvi; ii) Kuhamasisha na kuendeleza uvuvi na ukuzaji viumbe maji; iii) Kuweka miundombinu wezeshi ya uvuvi; na iv) Kuhamasisha uwekezaji katika Sekta ya Uvuvi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.

  91. 5.1.8.2. Wizara yenye dhamana ya Maji i) Kuhifadhi, kusimamia na kuendeleza vyanzo vya maji; na ii) Kusimamia matumizi endelevu na kufanya ufuatiliaji na tathmini ya rasilimali za maji. 17

  92. 5.1.8.3. Wizara yenye dhamana ya Kilimo na Umwagiliaji i) Kuhakikisha uwepo wa miundombinu wezeshi ya umwagiliaji; ii) Kuendeleza tafiti za teknolojia fanisi katika kilimo cha umwagiliaji; na iii) Kuhamasisha kilimo endelevu kinachohimili mabadiliko ya tabianchi.

  93. 5.1.8.4. Wizara yenye dhamana ya Nishati i) Kuhamasisha uwekezaji wa miradi ya kuzalisha umeme kwa kutumia maji; ii) Kuhamasisha na kufanya utafutaji, uendelezaji, uzalishaji na usimamizi wa mafuta na gesi asilia katika maeneo ya maji bahari na maji baridi; na iii) Kuhamasisha uzalishaji wa nishati mbadala kwa kutumia rasilimali za uchumi wa buluu.

  94. 5.1.8.5. Wizara yenye dhamana ya Uchukuzi i) Kudhibiti uchafuzi wa mazingira kutokana na shughuli za usafirishaji kwenye maji; ii) Kuhamasisha uwekezaji wa huduma za uchukuzi kwenye bahari na maziwa; na iii) Kutoa taarifa za hali ya hewa ili kuimarisha usalama wa vyombo vya usafiri kwa njia ya maji na watu;

  95. 5.1.8.6. Wizara yenye dhamana ya Madini i) Kuhamasisha na kuratibu tafiti za kijiolojia, utafutaji wa madini na matumizi ya teknolojia rafiki za uchimbaji wa madini kwenye maeneo ya maji; ii) Kujenga uwezo wa kitaasisi na utaalamu katika utafutaji na uchimbaji wa madini katika maeneo ya maji; na iii) Kuhamasisha uwekezaji katika utafutaji na uchimbaji endelevu wa madini katika maeneo ya maji.

  96. 5.1.8.7. Wizara yenye dhamana ya Maliasili na Utalii i) Kusimamia uhifadhi wa misitu ya pwani na fukwe za maji; ii) Kuendeleza utalii katika maeneo ya maji na fukwe; na iii) Kuhamasisha uwekezaji na ujenzi wa miundombinu wezeshi ya utalii katika maeneo ya maji na fukwe.

  97. 5.1.8.8. Wizara yenye dhamana ya Viwanda na Biashara i) Kuhamasisha na kuweka mazingira wezeshi ya biashara katika shughuli za Uchumi wa Buluu; 18 ii) Kuhamasisha uongezaji thamani wa bidhaa zitokanazo na shughuli za Uchumi wa Buluu; iii) Kuratibu upatikanaji wa masoko ya bidhaa zitokanazo na shughuli za Uchumi wa Buluu; na iv) Kuhamasisha uzalishaji wa bidhaa shindani kutokana na rasilimali za Uchumi wa Buluu.

  98. 5.1.8.9. Wizara yenye dhamana ya Ardhi Kupima ya Maeneo ya Maji.

  99. 5.1.8.10. Wizara yenye dhamana ya Katiba na Sheria Kutoa ushauri wa kisheria katika utekelezaji wa shughuli za Uchumi wa Buluu.

  100. 5.1.8.11. Wizara yenye dhamana ya Mambo ya Nje i) Kukuza ushirikiano na mataifa mengine na mashirikika ya kimataifa kwa ajili ya maendeleo endelevu ya uchumi wa buluu; na ii) Kutangaza fursa za uwekezaji katika Uchumi wa Buluu kimataifa.

  101. 5.1.8.12. Wizara yenye dhamana ya Ulinzi Kuhakikisha ulinzi wa mipaka kwenye maeneo ya rasilimali za Uchumi wa Buluu.

  102. 5.1.8.13. Wizara yenye dhamana na Mambo ya Ndani ya Nchi Kuratibu masuala ya usalama na jinai kwenye maeneo ya rasilimali za Uchumi wa Buluu.

  103. 5.1.8.14. Wizara yenye dhamana ya Ujenzi Kuratibu na kusimamia ujenzi wa miundombinu wezeshi katika sekta za Uchumi wa Buluu.

  104. 5.1.8.15. Wizara yenye dhamana ya Elimu, Sayansi na Teknolojia i) Kuijumuisha masuala ya Uchumi wa Buluu katika sera, mikakati, mipango, programu na mitaala ya elimu ya ngazi zote; na ii) Kuratibu masuala ya utafiti na teknolojia kuhusu matumizi na uendelezaji wa rasilimali za maji. 19

  105. 5.1.8.16. Wizara yenye dhamana ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum i) Kuhamasisha usawa wa kijinsia na kulinda ustawi na ushiriki wa wanawake na makundi maalumu katika usimamizi na uendelezaji wa rasilimali za Uchumi wa Buluu; na ii) Kuandaa, kusimamia na kuratibu utekelezaji wa kanuni, miongozo na programu zinazohamasisha kufikiwa kwa usawa wa kijinsia na uwezeshaji wanawake na makundi maalumu katika usimamizi na uendelezaji wa rasilimali za Uchumi wa Buluu;

  106. 5.1.8.17. Wizara yenye dhamana ya Sanaa na Michezo Kuhamasisha, kusimamia na kuimarisha uendelezaji wa shughuli za michezo kwenye maji.

  107. 5.1.8.18. Wizara yenye dhamana ya Afya i) Kuandaa, kusimamia na kuratibu utekelezaji wa kanuni, miongozo na programu zinazohamasisha jamii kujikinga na magonjwa yanayoambukiza ili yasiathiri shughuli za Uchumi wa Buluu; na ii) Kutoa elimu kwa umma kuhusu namna ya kujikinga na magonjwa yanayoambukiza ili yasiathiri shughuli za Uchumi wa Buluu.

  108. 5.1.8.19. Mamlaka ya Usimamizi wa Bahari Kuu i) Kuratibu, kusimamia na kuendeleza shughuli za Uchumi wa Buluu katika eneo la Ukanda Maalumu wa Uchumi wa Bahari na Bahari Kuu; ii) Kushirikiana na taasisi nyingine katika kuhamasisha uwekezaji katika eneo la Ukanda Maalumu wa Uchumi wa Bahari na Bahari Kuu; na iii) Kuimarisha ushiriki wa Tanzania katika taasisi na jumuiya za kikanda na kimataifa zinazojihusisha na Uchumi wa Buluu.

  109. 5.1.8.20. Sekta Binafsi i) Kutambua fursa na kuwekeza katika shughuli za uzalishaji za Uchumi wa Buluu; ii) Kuingia ubia na Serikali katika uwekezaji wa miradi ya pamoja ya Uchumi wa Buluu; na iii) Kushiriki na kutoa maoni katika Kamati mbalimbali za sekta za Uchumi wa Buluu. 20

  110. 5.1.8.21. Wadau wa Maendeleo Kusaidia juhudi za Serikali kupitia uwezeshaji wa misaada ya kiufundi, kiteknolojia na rasilimali fedha katika kutekeleza masuala ya Uchumi wa Buluu.

  111. 5.1.8.22. Asasi za Kiraia Kushiriki katika shughuli za Uchumi wa Buluu na kukuza uelewa kwa jamii kuhusu fursa zilizopo katika Uchumi wa Buluu.

  112. 5.1.8.23. Vyombo vya Habari i) Kutoa kwa wakati taarifa sahihi za fursa zitokanazo na rasilimali za Uchumi wa buluu kwa umma; na ii) Kushirikiana na Wizara za Kisekta kutekeleza programu za elimu kwa umma kuhusu masuala ya Uchumi wa buluu.

  113. 6.0 UFUATILIAJI NA TATHMINI Ufuatiliaji na tathmini utahusisha ukusanyaji na uchambuzi wa taarifa za utekelezaji wa Sera hii. Taarifa za ufuatiliaji zitatolewa kila mwaka na taarifa ya tathmini itatolewa kila baada ya miaka mitano ya utekelezaji wa Sera. Njia zitakazotumika kufuatilia utekelezaji wa Sera hii ni pamoja na: kufanya vikao vya mapitio ya mkakati wa utekelezaji wa Sera. Utaratibu wa ufuatiliaji na tathmini ya Sera umeainishwa katika Mkakati wa Utekelezaji wa Sera hii.

  114. 7.0 HITIMISHO Utekelezaji wa shughuli za Uchumi wa Buluu umekuwa ukifanyika kupitia sera, sheria, mikakati na mipango ya sekta za uvuvi, uchukuzi, maliasili na utalii, nishati, maji, viwanda, biashara, uwekezaji na kilimo cha umwagiliaji. Hata hivyo, Taifa halijanufaika ipasavyo kutokana na fursa zitokanazo na Uchumi wa Buluu. Hali hii inasababishwa na uwepo wa changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na: kukosekana kwa uratibu jumuishi wa wadau wanaosimamia sekta hizo; kukosekana kwa taasisi ya kusimamia baadhi ya shughuli zinazofanyika katika Ukanda Maalumu wa Uchumi wa Bahari na Bahari Kuu ikiwemo, utafutaji na uchimbaji wa mafuta, gesi asilia na madini chini ya maji; uwekezaji mdogo na usio wa kimkakati na fungamanishi katika matumizi ya rasilimali za Uchumi wa Buluu; na kuwepo kwa tafiti chache kwenye rasilimali za Uchumi wa Buluu. Aidha, Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo Endelevu (Rio+20) uliofanyika Rio de Janeiro nchini Brazil mwaka 2012 na Mkakati wa Afrika wa Uchumi wa Buluu wa Mwaka 2019 imeweka msukumo mkubwa katika kutambua matumizi endelevu ya 21 rasilimali za bahari na maji baridi katika misingi ya kiuchumi, kijamii na kimazingira. Vilevile, Ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020 na Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano 2021/22 - 2025/26 zinaelekeza Uchumi wa Buluu kupewa kipaumbele katika maendeleo ya nchi ili kukuza pato la nchi na wananchi kwa ujumla. Kwa msingi huo, Serikali imeamua kutunga Sera ya Taifa ya Uchumi wa Buluu ambayo ni nyenzo muhimu itakayowezesha nchi kutumia rasilimali za Uchumi wa Buluu ili kukuza uchumi wa Taifa kwa maendeleo endelevu. Sera hii haikusudii kuondoa sera, majukumu, sheria, mikakati ya sekta zenye mnasaba na Uchumi wa Buluu bali inakusudia kuchangia katika uimarishaji wa uratibu na kufungamanisha mipango na mikakati ya sekta hizo ili kuwa na tija zaidi katika uendelezaji na usimamizi wa shughuli za Uchumi wa Buluu hapa nchini. Aidha, ili kuendana na mahitaji ya Sera ya Taifa ya Uchumi wa Buluu ikiwemo kuboresha utekelezaji katika sekta, wizara za kisekta zinaweza kufanya mapitio ya sheria zake na kuzifanyia marekebisho pale itakapohitajika au kutungwa kwa sheria mpya. 22