跳到主要内容
Nelum
坦桑尼亚的法律

Kanuni za Msaada wa Kiufundi kwa Wamiliki wa Leseni Ndogo za Uchimbaji Madini za Mwaka 2025

文本截至 2026-09-28

以研究形式发布的公开法律与官方指引,不构成法律、税务或金融建议。

研究内容本身以英文撰写。标题和标签已翻译,调查结果和引文未翻译。

关于这部法律

类型
其他
编号
Tangazo la Serikali Na. 260 la tarehe 25/4/2025
颁布机构
Waziri wa Madini
国家
坦桑尼亚

在哪里阅读

文本

所收录的法律原文,按条款排列。每个条款都有自己的链接。

  1. 1. Jina.

  2. 2. Matumizi.

  3. 3. Tafsiri. SEHEMU YA PILI UTOAJI WA MSAADA WA KIUFUNDI KWA WAMILIKI WA LESENI NDOGO ZA UCHIMBAJI MADINI

  4. 4. Msaada wa kiufundi.

  5. 5. Idadi ya leseni za msaada wa kiufundi.

  6. 6. Wajibu wa afisa madini mkazi.

  7. 7. Wajibu wa mwezeshaji.

  8. 8. Wajibu wa mmiliki wa leseni.

  9. 9. Mgawanyo wa faida ya uwekezaji.

  10. 10. Usimamizi wa mgodi.

  11. 11. Uingizaji wa vifaa na mitambo.

  12. 12. Usalama na ulinzi wa eneo la leseni.

  13. 13. Muda wa mkataba.

  14. 14. Usajili wa mkataba.

  15. 15. Kurekebisha mkataba. 1 <!-- page break --> Kanuni za Msaada wa Kiufundi kwa Wamiliki wa Leseni Ndogo za Uchimbaji Madini Tangazo la Serikali Na.260 (Linaendelea.)

  16. 16. Kuvunja mkataba.

  17. 17. Lugha ya mkataba.

  18. 18. Notisi.

  19. 19. Sheria inayosimamia mkataba.

  20. 20. Utatuzi wa mgogoro SEHEMU YA TATU MASHARTI YA JUMLA

  21. 21. Usimamizi na ufuatiliaji wa mikataba.

  22. 22. Ukiukwaji. _______ JEDWALI _______ 2 <!-- page break --> Kanuni za Msaada wa Kiufundi kwa Wamiliki wa Leseni Ndogo za Uchimbaji Madini Tangazo la Serikali Na.260 (Linaendelea.) SHERIA YA MADINI, (SURA YA 123) ________ KANUNI ________ (Zimetengenezwa chini ya kifungu cha 129) KANUNI ZA MSAADA WA KIUFUNDI KWA WAMILIKI WA LESENI NDOGO ZA UCHIMBAJI MADINI ZA MWAKA 2025 Jina 1. Kanuni hizi zitajulikana kama Kanuni za Msaada wa Kiufundi kwa Wamiliki wa Leseni Ndogo za Uchimbaji Madini za Mwaka 2025. Matumizi 2. Kanuni hizi zitatumika kwa wamiliki wa leseni ndogo za uchimbaji madini. Tafsiri 3. Katika Kanuni hizi, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo- “afisa madini mkazi” maana yake ni afisa madini mkazi aliyeteuliwa chini ya kifungu cha 27 cha Sheria; “Katibu Mtendaji” maana yake ni Katibu Mtendaji aliyeteuliwa kwa mujibu wa Sheria; “mkataba” maana yake ni mkataba wa msaada wa kiufundi utakaoingiwa kati ya mmiliki wa leseni na mwezeshaji; “mmiliki wa leseni” maana yake ni mmiliki wa leseni ndogo ya uchimbaji madini; “msaada wa kiufundi” maana yake ni utaalamu wa uchimbaji, mitambo au mashine mbalimbali, namna ya uendeshaji wa mitambo, au ujuzi wa kufanya shughuli za madini usiopatikana nchini Tanzania, unaotolewa kwa lengo la kusaidia utafutaji, uchimbaji, uchenjuaji, ujuzi wa madini yanayokusudiwa kuchimbwa katika leseni ya uchimbaji mdogo kama ilivyoainishwa katika kifungu cha 8(3) cha Sheria; 3 <!-- page break --> Kanuni za Msaada wa Kiufundi kwa Wamiliki wa Leseni Ndogo za Uchimbaji Madini Tangazo la Serikali Na.260 (Linaendelea.) “mwezeshaji” maana yake ni mtu, kikundi cha watu au kampuni inayotoa msaada wa kiufundi kwa mmiliki wa leseni ndogo ya uchimbaji madini kwa mujibu wa kifungu cha 8(3) cha Sheria; Sura ya 123 “Sheria” maana yake ni Sheria ya Madini; “Tume” maana yake ni Tume ya Madini iliyoanzishwa chini ya Sheria; na “Waziri” maana yake ni Waziri mwenye dhamana ya masuala ya madini. SEHEMU YA PILI UTOAJI WA MSAADA WA KIUFUNDI KWA WAMILIKI WA LESENI NDOGO ZA UCHIMBAJI MADINI Msaada wa 4. Mmiliki wa leseni atapatiwa msaada wa kiufundi kiufundi kupitia mkataba wa maandishi utakaoingiwa kati yake na mwezeshaji. Idadi ya 5. Mmiliki wa leseni atakuwa na haki ya kuingia leseni za msaada wa mkataba wa kiufundi na mwezeshaji mmoja kwa leseni ndogo kiufundi za uchimbaji madini zisizozidi kumi kwa mkataba mmoja, kwenye eneo moja. Wajibu wa 6.-(1) Afisa madini mkazi atakuwa na wajibu wa-. afisa madini (a) kukagua leseni inayoombewa msaada wa mkazi kiufundi; (b) kubaini shughuli za uchimbaji madini zinazoendelea katika leseni na iwapo kuna migogoro yoyote; (c) kuhakiki iwapo mmiliki wa leseni ana madeni ya leseni au hati ya makosa katika ofisi nyingine za madini; (d) kubaini iwapo kuna migogoro yoyote ya kisheria, kiuendeshaji, au kikatiba inayohusu ombi husika iwapo leseni inamilikiwa na kikundi au kampuni; na (e) kuwasilisha kwa Katibu Mtendaji taarifa ya ukaguzi yenye ushauri na mapendekezo iwapo mmiliki wa leseni anastahili au hastahili kupata msaada wa kiufundi. 4 <!-- page break --> Kanuni za Msaada wa Kiufundi kwa Wamiliki wa Leseni Ndogo za Uchimbaji Madini Tangazo la Serikali Na.260 (Linaendelea.) (2) Taarifa itakayoandaliwa katika kanuni ndogo ya (1) itajumuisha taarifa zilizoainishwa katika Jedwali. Wajibu wa 7.-(1) Mwezeshaji atakuwa na wajibu ufuatao: mwezeshaji (a) kutoa msaada wa kiufundi kuhusu utafutaji wa madini, uchimbaji, mitambo, mashine mbalimbali, na utaalamu au ujuzi wa shughuli za madini na uchenjuaji wa madini; (b) kuhakikisha miundombinu yote isiyohamishika inazingatia kanuni na taratibu za utunzaji mazingira; (c) kuhakikisha kuwa vifaa anavyovitoa kwa mmiliki wa leseni vinakuwa sehemu ya mkataba na iwapo mkataba utakoma kutokana na sababu mbalimbali zilizobainishwa, mwezeshaji atakabidhi kwa mmiliki wa leseni vifaa vya utafiti, uchimbaji na uchenjuaji kama ilivyokubaliwa kwenye mkataba; (d) kwa kushauriana na mmiliki wa leseni, ataandaa mpango madhubuti wa urithishaji maarifa, ujuzi, utaalamu na matumizi ya teknolojia kwa TS. Na. watendaji wa mmiliki wa leseni kwa kuzingatia 305 la 2018 mahitaji kama ilivyobainishwa katika Mwongozo wa Tume wa Uwasilishaji wa Mpango wa Ushirikishwaji wa Wazawa kwenye Shughuli za Madini; (e) kwa kushirikiana na mmiliki wa leseni, kuandaa mpango madhubuti wa miradi ya wajibu wa wamiliki wa leseni kwa jamii; (f) kufanya utafiti katika eneo la leseni husika wakati uchimbaji wa madini unaendelea; (g) kuwasilisha mpango wa athari za kimazingira Sura ya 191 ulioidhinishwa na mamlaka husika kwa mujibu wa Sheria ya Mazingira kabla au ndani ya siku mia moja na ishirini baada ya kupata ridhaa ya Tume ya kuanza uchimbaji katika eneo la leseni; (h) kwa kushirikiana na mmiliki wa leseni, ataandaa mpango wa uchimbaji mgodi ambao utaidhinishwa kabla au ndani ya siku tisini baada ya kupata ridhaa ya Tume ya kuanza uchimbaji; 5 <!-- page break --> Kanuni za Msaada wa Kiufundi kwa Wamiliki wa Leseni Ndogo za Uchimbaji Madini Tangazo la Serikali Na.260 (Linaendelea.) TS. Na. (i) kuandaa mpango wa ufungaji mgodi na 408 la 2010 kuuwasilisha kwa mujibu wa utaratibu ulioainishwa kwenye Kanuni za Usalama Mahali pa Kazi, Afya na Utunzaji wa Mazingira; (j) kuandaa mpango wa utaratibu wa kubadilishana maarifa na taarifa za msingi kuhusu teknolojia inayotumika kwenye uzalishaji na shughuli za utafiti wa madini. (2) Mwezeshaji atakuwa na mwakilishi wa kudumu ambaye atahusika katika kutoa taarifa zote zinazohitajika katika mgodi pindi mamlaka husika itakapozihitaji. (3) Mipango iliyoandaliwa katika kanuni ndogo ya (1) itawasilishwa kwa afisa madini mkazi kama ifuatavyo: (a) kwa mipango iliyorejewa katika kanuni ndogo ya (1)(h), (i) na (j), itawasilishwa wakati wa maombi ya ridhaa au ndani ya siku tisini baada ya kupata ridhaa ya Tume ya kuanza kutoa msaada wa kiufundi; na (b) kwa mpango uliorejewa katika kanuni ndogo ya (1)(g), utawasilishwa wakati wa maombi ya ridhaa au ndani ya siku mia moja na ishirini baada ya kupata ridhaa ya Tume ya kuanza kutoa msaada wa kiufundi. (4) Bila kuathiri kanuni ndogo ya (1)(c), iwapo sababu za ukomo wa mkataba zinatokana na makusudi au uzembe wa mmiliki wa leseni kwa kutotimiza wajibu wake katika mkataba, na kwa kuzingatia masharti ya mkataba, mwezeshaji anaweza kuondoka na vifaa vyake ikiwa yeye hajasababisha au hajahusika moja kwa moja na vitendo vilivyosababisha kuvunjika kwa mkataba huo. Wajibu wa 8.-(1) Mmiliki wa leseni atakuwa na wajibu ufuatao: mmiliki wa leseni (a) kuzingatia Sheria na kanuni kuhusiana na taratibu za umiliki wa leseni na wajibu wake; (b) kutokuingia makubaliano na mtu mwingine kwa nia ya kutekeleza majukumu ya aina moja au yanayofanana kwa karibu na yale ambayo mwezeshaji anatakiwa kuyatimiza kwenye leseni husika katika kipindi cha uhai wa mkataba pasipo makubaliano na mwezeshaji; 6 <!-- page break --> Kanuni za Msaada wa Kiufundi kwa Wamiliki wa Leseni Ndogo za Uchimbaji Madini Tangazo la Serikali Na.260 (Linaendelea.) (c) kushiriki moja kwa moja katika usimamizi, uratibu, na utekelezaji wa shughuli zote za utafiti, uchimbaji, na uchenjuaji madini ndani ya eneo la leseni; (d) kuhakikisha shughuli zote za uchimbaji na uchenjuaji madini zinafanyika ndani ya eneo la leseni; (e) kwa kushirikiana na mwezeshaji, kuandaa mpango madhubuti wa miradi ya wajibu wa wamiliki wa leseni za madini kwa jamii; (f) kuhakikisha tozo, mrabaha na ada zote za Serikali zinazotokana na leseni zinalipwa kwa mujibu wa sheria; (g) kuhakikisha kuwa shughuli za uchimbaji zinafanyika kwa kuzingatia mpango wa usimamizi na utunzaji wa mazingira ulioidhinishwa; na (h) ikiwa ameruhusu mchimbaji au wachimbaji wengine kufanya shughuli za uchimbaji katika kitalu au vitalu mbalimbali ndani ya eneo la leseni, atalazimika kuwa na makubaliano ya maandishi na wamiliki wa vitalu hivyo yakibainisha haki na wajibu wao ikiwemo kufanya kazi kwa pamoja wakiwa na mwezeshaji au kulipwa fidia ili kusitisha kufanya shughuli katika vitalu husika na kumuacha mmiliki wa leseni aendelee kuchimba mwenyewe kwa msaada wa kiufundi kutoka kwa mwezeshaji. (2) Mpango na makubaliano ya maandishi yaliyoainishwa katika kanuni ndogo ya (1)(e) na (h) mtawalia, yatawasilishwa kwa afisa madini mkazi wakati wa uwasilishaji wa maombi ya ridhaa ya msaada wa kiufundi. Mgawanyo 9. Mkataba utakaoingiwa kati ya mwezeshaji na wa faida ya uwekezaji mmiliki wa leseni utazingatia masharti ya mgawanyo wa faida za mradi kwa utaratibu ufuatao: (a) mmiliki wa leseni atapata mgawanyo wa faida ghafi ya uzalishaji wa madini na makinikia usiopungua asilimia thelathini baada ya mrabaha, ada ya ukaguzi na tozo zote za Serikali kulipwa 7 <!-- page break --> Kanuni za Msaada wa Kiufundi kwa Wamiliki wa Leseni Ndogo za Uchimbaji Madini Tangazo la Serikali Na.260 (Linaendelea.) bila kujali gharama za uendeshaji wa mradi zilizoingiwa na mwezeshaji; na (b) endapo mmiliki wa leseni na mwezeshaji wataamua kuunganisha leseni ambazo zimeombewa msaada wa kiufundi kwa lengo la kupata leseni ya kati ya uchimbaji madini, watakubaliana kuhamisha leseni hiyo kwenda kampuni ya mwezashaji au kuanzisha kampuni ya ubia ili waweze kumiliki leseni ya kati ya uchimbaji madini kwa pamoja na kukubaliana kuhusu utaratibu wa mgawanyo wa faida za mradi kupitia leseni hiyo. Usimamizi 10.-(1) Usimamizi wa shughuli za mgodi utakuwa ni wa mgodi jukumu la pamoja kati ya mwezeshaji na mmiliki wa leseni. (2) Mmiliki wa leseni atakuwa na dhamana ya kusimamia na kuhakikisha kuwa sheria, kanuni na taratibu zinazingatiwa. (3) Wafanyakazi katika mgodi watakuwa raia wa Tanzania pekee isipokuwa katika masuala yanayohitaji msaada wa kiufundi kwa mujibu wa Kanuni hizi. (4) Bila kuathiri masharti ya kanuni ndogo ya (3), raia wa kigeni ataruhusiwa kufanya kazi katika eneo la leseni ndogo ya uchimbaji madini baada ya kukidhi matakwa ya sheria zinazohusiana na ajira kwa raia wa kigeni, na kabla ya raia huyo wa kigeni kuruhusiwa kuanza kufanya kazi katika eneo la leseni husika, mmiliki wa leseni atapaswa kuomba ridhaa kwa Tume ili raia huyo aruhusiwe kufanya kazi. Uingizaji 11.-(1) Mwezeshaji kwa kushirikiana na mmiliki wa wa vifaa na mitambo leseni atahakikisha kuwa vifaa na mitambo kwa ajili ya kutoa msaada wa kiufundi vinaingia katika eneo la mgodi na kutumika kwa ajili ya shughuli za uchimbaji madini zilizokusudiwa. (2) Mara baada ya vifaa na mitambo kuingia katika eneo la leseni, mmiliki wa leseni atatakiwa kutoa taarifa kwa afisa madini mkazi wa eneo husika kuhusu uwepo wa vifaa na mitambo hiyo. 8 <!-- page break --> Kanuni za Msaada wa Kiufundi kwa Wamiliki wa Leseni Ndogo za Uchimbaji Madini Tangazo la Serikali Na.260 (Linaendelea.) (3) Taarifa itakayotolewa na mmiliki wa leseni chini ya kifungu kidogo cha (2) itahusisha idadi na aina ya vifaa na mitambo. Usalama na 12. Mmiliki wa leseni na mwezeshaji watakuwa na ulinzi wa eneo la jukumu la kulinda usalama wa mali na eneo la leseni wakati leseni wote wa mkataba. Muda wa 13.-(1) Mkataba wa msaada wa kiufundi utakuwa wa mkataba kipindi kisichozidi miaka mitatu kuanzia tarehe ya kusajiliwa. (2) Mmiliki wa leseni, miezi mitatu kabla ya mkataba kufika ukomo, anaweza kuwasilisha kwa Tume maombi ya kuhuisha mkataba. (3) Bila kuathiri kanuni ndogo ya (1), uhuishaji wa mkataba unaweza kufanyika kwa kipindi kisichozidi jumla ya miaka kumi na mbili na kwa kuzingatia uhai wa leseni. Usajili wa 14.-(1) Mikataba ya msaada wa kiufundi mkataba itakayowasilishwa itahakikiwa na kusajiliwa na Tume. (2) Iwapo Tume itaamua kutosajili kkataba husika, itamjulisha mtu aliyewasilisha maombi kuhusu uamuzi huo. Kurekebish 15.-(1) Mmiliki wa leseni na mwezeshaji kwa pamoja a mkataba na kwa makubaliano ya maandishi wanaweza kurekebisha baadhi ya vifungu vya mkataba iwapo wataona inafaa. (2) Iwapo kutakuwa na mabadiliko ya sheria au kanuni ambayo yataathiri utekelezaji wa sehemu ya mkataba au mkataba wote, mwezeshaji na mmiliki wa leseni watajadiliana na kuingia makubaliano mapya kurekebisha sehemu ya mkataba iliyoathiriwa au kuhuisha mkataba wote ili kuendana na mabadiliko yaliyotokea. (3) Endapo yatagundulika madini mengine yenye thamani kiuchumi na mmiliki wa leseni akaomba kwa Tume kuongezewa madini hayo kwenye leseni yake na akakubaliwa, pande zote mbili za mkataba zitawajibika kufanya marekebisho kwenye mkataba wa awali au kuingia mkataba mpya na kuongeza mgawanyo wa faida za mradi kwa uwiano wataokubaliana. 9 <!-- page break --> Kanuni za Msaada wa Kiufundi kwa Wamiliki wa Leseni Ndogo za Uchimbaji Madini Tangazo la Serikali Na.260 (Linaendelea.) (4) Marekebisho yoyote yanayokusudiwa kufanyika katika mkataba yatawasilishwa kwa Tume kwa ajili ya kuridhiwa na kusajiliwa. Kuvunja 16. Kila upande utakuwa na haki ya kuvunja mkataba mkataba kwa kutoa notisi ya siku thelathini kutokana na sababu zifuatazo: (a) endapo upande mmoja hautaridhishwa na utekelezaji wa masharti ya mkataba; (b) kuisha kwa madini katika eneo la leseni linalohusika; (c) endapo upande mmoja utabaini vitendo vya udanyanyifu kama vile wizi wa madini, mitambo, vifaa na mali nyinginezo zilizopo mgodini na udaganyifu kuhusu ukokotoaji wa kiwango cha madini kilichozalishwa, au udanganyifu wa aina nyingine utakaoathiri utekelezaji wa mkataba; (d) endapo leseni itafutwa; na (e) endapo leseni itafikia ukomo na kutohuishwa. Lugha ya 17. Katika kuandaa mkataba wa msaada wa kiufundi, mkataba lugha ya mkataba itakuwa Kiswahili au Kiingereza. Notisi 18. Taarifa zote zinazohusu utekelezaji wa mkataba zitawasilishwa kwa wahusika wa mkataba kwa njia ya barua pepe, kwa mkono, au anuani ya posta, au njia nyingine ambayo watakubaliana. Sheria 19. Mkataba utakaoingiwa kati ya mmiliki wa leseni inayosima mia na mwezeshaji utatafsiriwa na utatekelezwa kwa mujibu wa mkataba Sheria za Tanzania. Utatuzi wa 20.-(1) Bila kuathiri masharti ya Sheria na Kanuni mgogoro hizi, endapo utatokea mgogoro kati ya mmiliki wa leseni na mwezeshaji katika utekelezaji wa mkataba, mgogoro huo utatatuliwa kwa njia ya mazungumzo ya amani. (2) Endapo pande zote zitashindwa kutatua mgogoro kwa njia ya mazungumzo ya amani, upande usioridhika 10 <!-- page break --> Kanuni za Msaada wa Kiufundi kwa Wamiliki wa Leseni Ndogo za Uchimbaji Madini Tangazo la Serikali Na.260 (Linaendelea.) utawasilisha mgogoro huo kwenye vyombo vya kisheria vyenye mamlaka. SEHEMU YA TATU MASHARTI YA JUMLA Usimamizi 21. Tume itakuwa na jukumu la kusimamia, kukagua, na ufuatiliaji na kufuatilia utekelezaji wa mikataba yote ya misaada ya wa kiufundi. mikataba Ukiukwaji 22. Mmiliki wa leseni ndogo ya uchimbaji madini anayekiuka masharti yaliyoainishwa chini ya Kanuni hizi atachukuliwa hatua kwa mujibu wa kifungu cha 63 cha Sheria. 11 <!-- page break --> Kanuni za Msaada wa Kiufundi kwa Wamiliki wa Leseni Ndogo za Uchimbaji Madini Tangazo la Serikali Na.260 (Linaendelea.) _______ JEDWALI ________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 6(2)) TAARIFA ZA UKAGUZI

  23. 1. Hali ya Maendeleo ya Leseni Katika sehemu hii, taarifa itaainisha- (a) jina la mmiliki na jina la mwezashaji, uraia na anuani yake, leseni, anuani na mahali leseni ilipo; (b) idadi na namba za leseni zinazohusika kwa mkataba wa msaada wa kiufundi; (c) tarehe ya kusainiwa kwa mkataba wa msaada wa kiufundi; (d) shughuli za madini zilizotekelezwa katika eneo la leseni kuanzia tarehe ya kutolewa leseni; (e) maendeleo yaliyofanyika katika eneo la leseni kulingana na matakwa ya Sheria; (f) uhusiano uliopo kati ya mmiliki wa leseni na wachimbaji wengine wenye vitalu ndani ya eneo la leseni; na (g) makubaliano yaliyofikiwa ya kufanya shughuli za madini kati ya mmiliki wa leseni na wachimbaji wadogo wenye maduara ndani ya eneo la leseni.

  24. 2. Vibali au idhini iliyotolewa Katika sehemu hii, taarifa itaainisha- (a) iwapo mpango wa utafutaji na uchimbaji wa madini umeandaliwa, umewasilishwa na au umeidhinishwa na Tume; na (b) iwapo mpango wa usimamizi wa mazingira umeandaliwa, umewasilishwa na au umeidhinishwa na mamlaka husika.

  25. 3. Urithishaji wa ujuzi na teknolojia kwa mmiliki wa leseni na wafanyakazi wake Katika sehemu hii, taarifa itaainisha- (a) iwapo mpango wa urithishaji wa teknolojia, ujuzi na matumizi ya teknolojia kwa mmiliki wa leseni na wafanyakazi wake unatekelezeka; na (b) iwapo mpango wa utaratibu wa kubadilishana maarifa na taarifa za msingi kuhusu teknolojia inayotumika kwenye uzalishaji na shughuli za utafiti wa madini unatekelezeka.

  26. 4. Utekelezaji wa miradi ya wajibu wa wamiliki wa leseni kwa jamii| Sehemu hii itaainisha kuhusu mpango wa wajibu wa mmiliki wa leseni kwa jamii kulingana na matakwa ya Sheria na Kanuni za Wajibu wa Wamiliki wa Leseni za Madini kwa Jamii.

  27. 5. Changamoto zinazomkabili mmiliki wa leseni Katika sehemu hii, taarifa itaainisha- (a) aina ya changamoto zinazomkabili mmiliki wa leseni; na 12 <!-- page break --> Kanuni za Msaada wa Kiufundi kwa Wamiliki wa Leseni Ndogo za Uchimbaji Madini Tangazo la Serikali Na.260 (Linaendelea.) (b) hatua zilizochukuliwa kutatua changamoto hizo.

  28. 6. Mapendekezo Katika sehemu hii, taarifa inapaswa kuainisha mapendekezo ya kitaalamu yatakayobainisha iwapo mmiliki wa leseni anastahili kupatiwa msaada wa kiufundi au la. Dodoma, ANTHONY PETER MAVUNDE, 17 Aprili, 2025 Waziri wa Madini 13 <!-- page break -->

Kanuni za Msaada wa Kiufundi kwa Wamiliki wa Leseni Ndogo za Uchimbaji Madini za Mwaka 2025 · Nelum