Taarifa kwa Umma: Mpango wa Ununuzi wa Dhahabu Nchini (08 Oktoba 2024)
文本截至 2026-09-29
以研究形式发布的公开法律与官方指引,不构成法律、税务或金融建议。
研究内容本身以英文撰写。标题和标签已翻译,调查结果和引文未翻译。
关于这部法律
- 类型
- 其他
- 编号
- BoT press release file 2024100812030421
- 颁布机构
- Bank of Tanzania (Gavana)
- 国家
- 坦桑尼亚
在哪里阅读
文本
所收录的法律原文,按条款排列。每个条款都有自己的链接。
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA BENKI KUU YA TANZANIA 08 Oktoba 2024 TAARIFA KWA UMMA MPANGO WA UNUNUZI WA DHAHABU NCHINI Benki Kuu ya Tanzania inapenda kutoa taarifa kuhusu Mpango wa Ununuzi wa Dhahabu Nchini. Mpango huu unatoa fursa kwa wauzaji wa dhahabu kuuza dhahabu zao moja kwa moja kwa Benki Kuu ya Tanzania kwa bei ya ushindani ya soko la kimataifa. Chini ya mpango huu, wauzaji wa dhahabu watapata punguzo la ada na uhakika wa malipo ya haraka wakiuza asilimia 20 ya dhahabu zao Benki Kuu kama ilivyoainishwa katika kifungu cha 59 cha Sheria ya Madini (Sura ya 123). Kwa siku ya leo, tarehe 08 Oktoba 2024, Benki Kuu inanunua dhahabu kwa TZS 233,372.14 kwa gramu moja. Taarifa zaidi: i. Bei: Bei itakayotumika ni bei ya dhahabu duniani kama inavyotolewa na Tume ya Madini, hivyo bei hubadilika kila siku; ii. Malipo: Asilimia 100 ya malipo baada ya kupokea ripoti ya uchenjuaji wa dhahabu; iii. Muda wa malipo: Ndani ya masaa 24 baada ya kupata ripoti ya uchenjuaji; iv. Gharama za kuchenjua: Benki Kuu italipia asilimia 100 ya gharama za kuchenjua dhahabu; v. Asilimia 20 ya dhahabu: Hii inahusu mmiliki wa leseni ya uchimbaji wa madini na mfanyabiashara mkubwa wa madini; vi. Motisha: Mrabaha asilimia 4 badala ya asilimia 6; Ada ya ukaguzi ni asilimia 0 badala ya asilimia 1; na Kodi ya Ongezeko la Thamani asilimia 0, hivyo muuzaji wa dhahabu anaweza kudai “input tax”; na vii. Chini ya mpango huu, wamiliki wa leseni ya uchimbaji wa madini, wafanyabiashara wakubwa wa madini na viwanda vya kuchenjulia dhahabu wanaweza kuiuzia Benki Kuu kiasi chochote cha dhahabu. Wauzaji wa dhahabu wanapaswa kuwasilisha dhahabu yao katika mojawapo ya viwanda vifuatavyo vya uchenjuaji wa dhahabu: Geita Gold Refinery Ltd, Mwanza Precious Metals Refinery Co. Ltd na Eyes of Africa Ltd. Kwa taarifa na ufafanuzi zaidi, tafadhali usisite kuwasiliana na Benki Kuu ya Tanzania. GAVANA BENKI KUU YA TANZANIA <!-- page break -->