Kanuni za Madini (Ufifilishaji wa Makosa) za Mwaka 2022
Text as of 2026-09-28
Public law and official guidance, published as research. Not legal, tax or financial advice.
About this law
- Kind
- Other
- Number
- Tangazo la Serikali Na. 549 la tarehe 2/9/2022
- Issued by
- Waziri wa Madini
- Country
- Tanzania
Where to read it
Text
The law's own text, section by section, as held. Each section has its own link.
1. Jina.
2. Tafsiri. SEHEMU YA PILI UTARATIBU WA KUFIFILISHA MAKOSA PAMOJA NA KUKAZIA AMRI YA UFIFIFLISHAJI
3. Utaratibu wa kufifilisha kosa.
4. Ulipaji wa fedha kwa kosa lililofifilishwa.
5. Utaratibu wa kukazia amri ya ufifilishaji.
6. Utunzaji wa fedha zinazotokana na ufifilishaji wa makosa. SEHEMU YA TATU MASHARTI YA JUMLA
7. Mamlaka ya Tume.
8. Taarifa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka. 1 <!-- page break --> Kanuni za Madini (Ufifilishaji wa Makosa) Tangazo la serikali na. 549 (linaendelea) ________ JEDWALI ________ SHERIA YA MADINI, (SURA YA 123) _______ KANUNI _______ (Zimetengenezwa chini ya kifungu cha 132A(7)) KANUNI ZA MADINI (UFIFILISHAJI WA MAKOSA) ZA MWAKA 2022 SEHEMU YA KWANZA MASHARTI YA UTANGULIZI Jina 1. Kanuni hizi zitajulikana kama Kanuni za Madini (Ufifilishaji wa Makosa) za Mwaka 2022. Tafsiri 2. Katika Kanuni hizi, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo- “Katibu Mtendaji” maana yake ni Katibu Mtendaji aliyeteuliwa chini ya kifungu cha 24 cha Sheria; “ofisa aliyeidhinishwa” maana yake ni ofisa aliyeidhinishwa kama ilivyotafsiriwa chini ya kifungu cha 4 cha Sheria; “Tume” maana yake ni Tume ya Madini iliyoanzishwa chini ya Sheria; na “ufifilishaji wa makosa” maana yake ni mchakato ambao unamwezesha mtu aliyetenda kosa kuwasilisha maombi yake kwa maandishi kwenye chombo chenye mamlaka ya ufifilishaji wa makosa akikiri kutenda kosa na hivyo kuwa na hiari ya kulipa kiasi kilichofifilishwa badala ya kushtakiwa mahakamani. 2 <!-- page break --> Kanuni za Madini (Ufifilishaji wa Makosa) Tangazo la serikali na. 549 (linaendelea) SEHEMU YA PILI UTARATIBU WA KUFIFILISHA MAKOSA PAMOJA NA KUKAZIA AMRI YA UFIFILISHAJI Utaratibu wa 3.-(1) Endapo mtu ametenda kosa chini ya Sheria na kufifilisha kosa Katibu Mtendaji au ofisa aliyeidhinishwa akaamua kufifilisha kosa hilo, atamfahamisha mtu huyo kuhusu uamuzi huo kwa namna ambayo imeainishwa katika fomu ya taarifa ya kosa KMUM-1 iliyoainishwa katika Jedwali. (2) Mtu aliyepokea taarifa chini ya kanuni ndogo ya (1), ndani ya saa ishirini na nne, atatakiwa kukiri kosa kwa maandishi na kukubali kulipa kiasi cha fedha kama adhabu ya kosa lililofifilishwa au kueleza nia yake ya kujitetea mahakamani kuhusu shtaka lake. (3) Mtu ambaye amepokea taarifa ya kosa na kukiri kosa hilo atajaza fomu ya kukiri kosa KMUM-2 iliyoainishwa katika Jedwali. (4) Bila kujali kanuni ndogo ya (2), Katibu Mtendaji au ofisa aliyeidhinishwa anaweza, endapo kuna sababu za msingi, kuruhusu mtu kukiri kosa baada ya kupita kwa kipindi cha saa ishirini na nne lakini kukiri huko kunapaswa kufanyika kabla ya shauri kufunguliwa mahakamani. (5) Endapo kosa linalohusisha ukamataji wa madini, taarifa ya kosa itaambatishwa na fomu ya ukamataji iliyojazwa ipasavyo kupitia fomu KMUM-3 iliyoainishwa kwenye Jedwali. (6) Taarifa ya kosa iliyorejewa katika kanuni ndogo ya (1)- (a) itataja kosa mahsusi lililotendwa na kifungu kilichokiukwa; (b) itakuwa na maelezo mafupi ya kosa; (c) itabainisha kiasi cha faini kwa kosa lililotendeka kama kilivyotajwa kwenye Sheria na kiasi cha fedha kinachotakiwa kulipwa baada ya kufifilishwa kwa kosa hilo; (d) itaeleza endapo mtu aliyetenda kosa amechagua kujaza fomu ya kukiri kosa au amejaza fomu ya 3 <!-- page break --> Kanuni za Madini (Ufifilishaji wa Makosa) Tangazo la serikali na. 549 (linaendelea) kuwa na nia ya kujibu shtaka Mahakamani; na (e) itasainiwa na kuwekwa tarehe na Katibu Mtendaji au ofisa aliyeidhinishwa kwa upande mmoja na mtu aliyetenda kosa kwa upande mwingine. Ulipaji wa fedha 4.-(1) Mtu ambaye anakiri kutenda kosa, atatakiwa kwa kosa lililofifilishwa kulipa kiasi cha fedha kilichotajwa katika fomu ya taarifa ya kosa ndani ya siku saba kutoka tarehe ambayo amekiri kosa hilo. (2) Bila ya kujali kanuni ndogo ya (1), malipo yanaweza kufanyika kwa namna ambayo Katibu Mtendaji au ofisa aliyeidhinishwa ataelekeza. (3) Endapo mtu aliyekiri kosa hatalipa kiasi cha fedha kilichotozwa kama adhabu kwa kosa lililofifilishwa ndani ya kipindi kilichotajwa katika fomu ya kukiri kosa, Tume itakuwa inamtoza riba ya asilimia tano ya kiasi cha fedha kilichotozwa kwa kila mwezi. Utaratibu wa 5. Endapo mtu atashindwa kulipa kiasi cha fedha kukazia amri ya ufifilishaji kilichotozwa kama adhabu kwa kosa lililofifilishwa pamoja na riba iliyotokana na kiasi hicho katika kipindi cha siku tisini masharti ya Sheria kuhusu ufifilishaji wa makosa yatatumika. Utunzaji wa 6. Fedha zote zinazokusanywa kutokana na ufifilishaji fedha zinazotokana na wa makosa zitatakiwa kuhifadhiwa katika Mfuko Mkuu wa ufifilishaji wa Serikali isipokuwa kama Waziri mwenye dhamana na fedha makosa ataelekeza vinginevyo. SEHEMU YA TATU MASHARTI YA JUMLA Mamlaka ya 7. Utekelezaji wa mamlaka kuhusu ufifilishaji wa Tume makosa hautaathiri mamlaka ya Tume au chombo kingine kuhusiana na ukamataji wa madini na kifaa au kitu chochote ambacho kinahusiana na afya mahali pa kazi, usalama na usimamizi wa mazingira. Taarifa kwa 8.-(1) Katibu Mtendaji atawasilisha taarifa kuhusu Mkurugenzi wa Mashtaka makosa yaliyofifilishwa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka ndani 4 <!-- page break --> Kanuni za Madini (Ufifilishaji wa Makosa) Tangazo la serikali na. 549 (linaendelea) ya siku kumi na tano baada ya kila robo ya mwaka. (2) Taarifa itakayowasilishwa chini ya kanuni ndogo ya (1) itajumuisha yafuatayo: (a) jina na taarifa za mtuhumiwa; (b) kosa lililotendwa pamoja na kifungu kilichokiukwa; (c) tarehe na mahali ambako kosa limetendwa; (d) kiasi cha fedha kilichotozwa kama adhabu kwa kosa lililofifilishwa kikijumuisha na riba, kama ipo; (e) maelezo kuhusu hali ya malipo ya fedha iliyotozwa kama adhabu kwa kosa lililofifilishwa; na (f) taarifa nyingine yoyote muhimu kadri Mkurugenzi wa Mashataka atakavyohitaji. ________ JEDWALI ________ 5 <!-- page break --> Kanuni za Madini (Ufifilishaji wa Makosa) Tangazo la serikali na. 549 (linaendelea) ________ JEDWALI ________ KMUM-1 FOMU YA TAARIFA YA KOSA (Imetengenezwa chini ya kanuni ya 3(1)) Kwa………………………………………………………………..Anwani……………………………… …
1. Unashtakiwa kwa kosa/makosa kama ifuatavyo: (a) …………………………………..kinyume na…………………..cha/ya………………….. (b) …………………………………..kinyume na…………………..cha/ya………………….. (c) …………………………………..kinyume na…………………..cha/ya………………….. (d) …………………………………..kinyume na…………………..cha/ya…………………..
2. Endapo unakiri kosa utajaza “FOMU YA KUKIRI KOSA” iliyoambatishwa hapa na kuirudisha ikiwa pamoja na taarifa hii kwa Katibu Mtendaji/ofisa aliyeidhinishwa ndani ya saa ishirini na nne kutoka muda ulipopata taarifa hii.
3. Kwa kosa/makosa yaliyotajwa katika aya ya 1 ya taarifa hii utapaswa kulipa kiasi cha shilingi………………kama adhabu ya kosa/makosa yaliyofifilishwa: S/N KOSA/MAKOSA FAINI KWA KIASI CHA FAINI MUJIBU WA KILICHOFIFILISHWA SHERIA 6 <!-- page break --> Kanuni za Madini (Ufifilishaji wa Makosa) Tangazo la serikali na. 549 (linaendelea) IMETOLEWA NA: IMEPOKELEWA NA: NAME:……………………… NAME……………… SAINI……………………….. SAINI………………... CHEO……………………….. UHUSIKA……………. TAREHE.…………………... TAREHE…………… KMUM-2 FOMU YA KUKIRI KOSA (Imetengenezwa chini ya kanuni ya 3(3)) Mimi……………………………. wa…………………………………..(anwani ya makazi au biashara) nikiwa mmiliki/mkurugenzi/meneja/mwakilishi wa…………………………(jina la kampuni/ubia, n.k) nakiri kosa katika shtaka/mashtaka ya……………………………………………yaliyoainishwa kwenye Fomu ya Taarifa ya Kosa. Naomba kosa nililotenda lifanyiwe ufifilishaji kwa mujibu wa Sheria ya Madini. Naahidi kuwa nitalipa kiasi cha fedha kilichoainishwa kama adhabu ya kosa litakalofifilishwa ambacho ni shilingi……………………………….ndani ya siku saba kutoka leo tarehe ……………….. 7 <!-- page break --> Kanuni za Madini (Ufifilishaji wa Makosa) Tangazo la serikali na. 549 (linaendelea) Natambua kwamba riba ya asilimia tano kwa kila mwezi itatozwa endapo sitalipa kiasi cha fedha kilichotajwa ndani ya muda uliotajwa hapo juu. Saini ya mtu aliyepewa taarifa ya kosa…………………………………………………………………… Tarehe......……………………………………………………………………………………… …………... Saini ya Katibu Mtendaji/Ofisa Aliyeidhinishwa……………………………………………………… Tarehe………………………………………………………………………………………… …... 8 <!-- page break --> Kanuni za Madini (Ufifilishaji wa Makosa) Tangazo la serikali na. 549 (linaendelea) KMUM-3 JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MADINI TUME YA MADINI FOMU YA KUKAMATA MADINI (MINERALS SEIZURE FORM) (Imetengenezwa chini ya kanuni ya 3(5)) TAARIFA ZA ALIYEKAMATWA NA MC/MS NO. MADINI/ PERSONAL DETAILS Jina la Jina la Jina la Ukoo Kwanza Kati Middle Surname First Name Name Kitamb Aina ya Utaifa ulisho Kitambulisho Tarehe National Date of ID No. ID Type ity Issue Anwan Namba ya i Simu Addres Telephone s No. Barua Saini Pepe Email Signature MAELEZO YA TUKIO/ INCIDENT DETAILS Tare Mu Mahali he da Tim Locatio Date e n MADINI YALIYOKAMATWA/ SEIZED MINERALS Na. Maelezo ya Madini Yaliyokamatwa/ Uzito/ Maoni/ Remarks (S/N) Description of Seized Minerals Weight 1. 2. 3. 4. 5. SABABU ZA KUKAMATWA KWA MADINI/ REASONS FOR MINERAL SEIZURE 9 <!-- page break --> Kanuni za Madini (Ufifilishaji wa Makosa) Tangazo la serikali na. 549 (linaendelea) Madini yaliyotajwa hapo juu yameshikiliwa kwa muda na Afisa wa Tume ya Madini kwa niaba ya Tume ya Madini kulingana na vifungu vya sheria na kanuni zifuatazo (The above-mentioned minerals have been temporarily seized by the Mining Commission Officer from the offender in contravening the following):
1. Kifungu Na. 6(4) cha Sheria ya Madini Sura ya 123 (Section 6(4) of the Mining Act Cap 123)
2. Kifungu Na. 18(1) cha Sheria ya Madini Sura ya 123 (Section 18(1) of the Mining Act Cap 123)
3. Kifungu Na. 18(3) cha Sheria ya Madini Sura ya 123 (Section 18(3) of the Mining Act Cap 123)
4. Kifungu Na. 91(1) cha Sheria ya Madini Sura ya 123 (Section 91(1) of the Mining Act Cap 123)
5. Kifungu Na. 6(1) cha Kanuni za Masoko ya Madini (2019) (Section 6(1) of the Mining (Mineral and Gem Houses) Regulations)
6. Kifungu Na. 10(1) cha Kanuni za Biashara ya Madini na Makinikia ya Madini (Section 10(1) of the Mining (Mineral and Mineral Concentrates Trading) Regulations)
7. Kifungu Na. 10(2) cha Kanuni za Biashara ya Madini na Makinikia ya Madini (Section 10(2) of the Mining (Mineral and Mineral Concentrates Trading) Regulations)
8. Kifungu Na. 10(3) cha Kanuni za Biashara ya Madini na Makinikia ya Madini (Section 10(3) of the Mining (Mineral and Mineral Concentrates Trading) Regulations) UFUNGAJI WA LAKIRI/ SEALING Madini tajwa hapo juu yamekaguliwa na Afisa wa Tume ya Madini na kufungwa kwenye mfuko maalum mbele ya mtajwa hapo juu na mashahidi kwa lakiri namba (The above listed minerals has been verified by the Mining Commission Officer in presence of the aforementioned and witnesses): Lakiri Na. 1 Lakiri Na. 3 (Seal No. 1) (Seal No. 3) Lakiri Na. 2 Lakiri Na. 4 (Seal No. 2) (Seal No. 4) USHAHIDI/WIT NESSING Shahidi/ Witness Jina Kamili/ Full Name Simu/ Telephone No. Saini/ Signature Shuhuda wa Mtuhumiwa Offender Witness Shuhuda wa Serikali Government Witness Afisa wa Tume ya Madini Mining Commission Officer Dodoma, DOTO MASHAKA BITEKO 26th Augost, 2022 Waziri wa Madini 10 <!-- page break -->