Taarifa kwa Umma: Mpango wa Ununuzi wa Dhahabu Nchini (07 Oktoba 2024)
Text as of 2026-09-28
Public law and official guidance, published as research. Not legal, tax or financial advice.
About this law
- Kind
- Other
- Number
- BoT press release file 2024100717352414
- Issued by
- Bank of Tanzania (Gavana)
- Country
- Tanzania
Where to read it
Text
The law's own text, section by section, as held. Each section has its own link.
<!-- page 1 --> hi ce ” za JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA | : NA BENKI KUU YA TANZANIA 2 | g Repu we Re 07 Oktoba 2024 TAARIFA KWA UMMA MPANGO WA UNUNUZI WA DHAHABU NCHINI Benki Kuu ya Tanzania inapenda kutoa taarifa kuhusu Mpango wa Ununuzi wa Dhahabu Nchini. Mpango huu unatoa fursa kwa wauzaji wa dhahabu kuuza dhahabu zao moja kwa moja kwa Benki Kuu ya Tanzania kwa bei ya ushindani ya soko la kimataifa. Chini ya mpango huu, wauzaji wa dhahabu watapata punguzo la ada na uhakika wa malipo ya haraka wakiuza asilimia 20 ya dhahabu zao Benki Kuu kama ilivyoainishwa katika kifungu cha 59 cha Sheria ya Madini (Sura ya 123). Kwa siku ya leo, tarehe 07 Oktoba 2024, Benki Kuu inanunua dhahabu kwa TZS 234,703.95 kwa gramu moja. Taarifa zaidi: i. Bei: Bei itakayotumika ni bei ya dhahabu duniani kama inavyotolewa na Tume ya Madini, hivyo bei hubadilika kila siku; ii. Malipo: Asilimia 100 ya malipo baada ya kupokea ripoti ya uchenjuaji wa dhahabu; iii. Muda wa malipo: Ndani ya masaa 24 baada ya kupata ripoti ya uchenjuaji. Kwa miamala ya tarehe 02 Oktoba 2024, malipo yalifanyika ndani ya masaa sita; iv. Gharama za kuchenjua: Benki Kuu italipia asilimia 100 ya gharama za kuchenjua dhahabu; v. Asilimia 20 ya dhahabu: Hii inahusu mmiliki wa leseni ya uchimbaji wa madini na mfanyabiashara mkubwa wa madini; vi. Motisha: Mrabaha asilimia 4 badala ya asilimia 6; Ada ya ukaguzi ni asilimia 0 badala ya asilimia 1; na Kodi ya Ongezeko la Thamani asilimia 0, hivyo muuzaji wa dhahabu anaweza kudai “input tak”; na vii. Chini ya mpango huu, wamiliki wa leseni ya uchimbaji wa madini, wafanyabiashara wakubwa wa madini na viwanda vya kuchenjulia dhahabu wanaweza kuiuzia Benki Kuu kiasi chochote cha dhahabu. Wauzaji wa dhahabu wanapaswa kuwasilisha dhahabu yao katika mojawapo ya viwanda vifuatavyo vya uchenjuaji wa dhahabu: Geita Gold Refinery Ltd, Mwanza Precious Metals Refinery Co. Ltd na Eyes of Africa Ltd. Kwa taarifa na ufafanuzi zaidi, tafadhali usisite kuwasiliana na Benki Kuu ya Tanzania. GAVANA BENKI KUU YA TANZANIA