Skip to content
Nelum
Laws of Tanzania

Taarifa kwa Umma: Mpango wa Ununuzi wa Dhahabu Nchini (dated 01 Oktoba 2024)

Text as of 2026-09-29

Public law and official guidance, published as research. Not legal, tax or financial advice.

About this law

Kind
Other
Number
BoT press release file 2024100206312714
Issued by
Bank of Tanzania (Gavana)
Country
Tanzania

Where to read it

Text

The law's own text, section by section, as held. Each section has its own link.

  1. JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA BENKI KUU YA TANZANIA 01 Oktoba 2024 TAARIFA KWA UMMA MPANGO WA UNUNUZI WA DHAHABU NCHINI Benki Kuu ya Tanzania inapenda kutoa taarifa kuhusu Mpango wa Ununuzi wa Dhahabu Nchini. Mpango huu unatoa fursa kwa wauzaji wa dhahabu kuuza dhahabu zao moja kwa moja kwa Benki Kuu ya Tanzania kwa bei ya ushindani ya soko la kimataifa. Chini ya mpango huu, wauzaji wa dhahabu watapata punguzo la ada na uhakika wa malipo ya haraka wakiuza asilimia 20 ya dhahabu zao Benki Kuu kama ilivyoainishwa katika kifungu cha 59 cha Sheria ya Madini (Sura ya 123). Bei na ada za ununuzi wa dhahabu kwa tarehe 1 Oktoba 2024 Maelezo Kiasi Bei kwa gramu (kabla ya makato)** TZS 232,876.89 Mrabaha 4% (TZS 9,315.08) Ada ya ukaguzi 0% (TZS 0) Jumla kwa gramu TZS 223,561.81 **bei zinabadilika kila siku Taarifa muhimu: i. Bei: Bei itakayotumika ni bei ya dhahabu duniani kama inavyotolewa kila siku na Tume ya Madini; ii. Malipo: Asilimia 100 ya malipo baada ya kupokea ripoti ya uchenjuaji wa dhahabu; iii. Muda wa malipo: Ndani ya masaa 24 baada ya kupata ripoti ya uchenjuaji; iv. Gharama za kuchenjua: Benki Kuu italipia asilimia 100 ya gharama za kuchenjua dhahabu; v. Asilimia 20 ya dhahabu: Hii inahusu mmiliki wa leseni ya uchimbaji wa madini na mfanyabiashara mkubwa wa madini; vi. Motisha: Mrabaha asilimia 4 badala ya asilimia 6; Ada ya ukaguzi ni asilimia 0 badala ya asilimia 1; na Kodi ya Ongezeko la Thamani asilimia 0, hivyo muuzaji wa dhahabu anaweza kudai “input tax”; na vii. Chini ya mpango huu, wamiliki wa leseni ya uchimbaji wa madini, wafanyabiashara wakubwa wa madini na viwanda vya kuchenjulia dhahabu wanaweza kuiuzia Benki Kuu kiasi chochote cha dhahabu. Benki Kuu inahimiza wauzaji wote wa dhahabu kutumia fursa hii ili kuongeza thamani ya dhahabu zao na malipo ya uhakika na ya haraka wakati wote. Kwa taarifa na ufafanuzi zaidi, tafadhali usisite kuwasiliana na Benki Kuu ya Tanzania. GAVANA BENKI KUU YA TANZANIA <!-- page break -->

Taarifa kwa Umma: Mpango wa Ununuzi wa Dhahabu Nchini (dated 01 Oktoba 2024) · Nelum