تخطَّ إلى المحتوى
Nelum
قوانين تنزانيا

Mwongozo wa Ununuzi wa Dhahabu (Toleo la Agosti 2024) with covering minute

النص بتاريخ 2026-09-28

القانون العام والإرشادات الرسمية منشورة بوصفها أبحاثاً. ليست مشورة قانونية أو ضريبية أو مالية.

البحث نفسه مكتوب بالإنجليزية. العناوين والوسوم مترجمة؛ أما النتائج والاقتباسات فغير مترجمة.

عن هذا القانون

النوع
أخرى
الرقم
Commission minute of 16/08/2024
الجهة المصدرة
Mining Commission (Acting Executive Secretary Eng. Ramadhani M. Lwamo)
الدولة
تنزانيا

أين تقرؤه

النص

نص القانون نفسه، مادةً مادة، كما هو محفوظ. لكل مادة رابطها.

  1. 1. Vigezo vya kutenga a) Mmiliki wa leseni ya uchimbaji wa madini na madini mfanyabiashara mkubwa wa madini atatenga asilimia isiyopungua 20 ya madini yote ya dhahabu aliyonayo kwa ajili ya kusafishwa na kuuzwa ndani ya nchi; b) Madini ya dhahabu yaliyotengwa yatauzwa kwa Serikali (kupitia Benki Kuu ya Tanzania) na viwanda vya kusafisha dhahabu; .C) Haki ya kipekee ya kununua madini ya dhahabu yaliyotengwa itakuwa kwa Serikali (Benki Kuu ya Tanzania); d) Mmiliki wa leseni ya uchimbaji wa madini na mfanyabiashara mkubwa wa madini atawajibika kupeleka madini ya dhahabu aliyotenga kwa mujibu wa sheria katika mojawapo ya viwanda vya kusafisha dhahabu vilivyobainishwa baada ya kupewa kibali cha kusafirisha madini na Tume ya Madini kwa lengo la kuiuzia Benki Kuu ya Tanzania au kiwanda cha kusafisha dhahabu; e) Iwapo Benki Kuu ya Tanzania haitakuwa na nia ya kununua dhahabu kwa kipindi husika, Benki Kuu itaijulisha Tume ya Madini kwa maandishi kupitia waraka walau mwezi mmoja kabla ya tarehe ya kuacha kununua dhahabu iliyotengwa kwa mujibu wa sheria, dhahabu itakayokuwa inaendelea kutengwa itauzwa kwa wamiliki wa viwanda vya kusafisha madini ya dhahabu nchini; f) Mara baada ya kupokea waraka wa Benki Kuu ya Tanzania kuhusu uamuzi wa kutoendelea na ununuzi wa dhahabu, Tume ya Madini itasambaza waraka huo kwa wamiliki wa leseni za uchimbaji wa madini na wafanyabiashara wakubwa wa madini ili wauze madini waliyotenga katika viwanda vya kusafisha madini ya dhahabu nchini; na 9) Benki Kuu ya Tanzania itaijulishaTume ya Madini kupitia waraka kuhusu tarehe ya kuanza tena kununua dhahabu baada ya kusitisha ununuzi huo. Tume ya Madini itasambaza waraka wenye 3 <!-- page 5 --> HOUR AA i i as ee tarehe ya kuanza kwa ununuzi wa dhahabu kwa ee

  2. 2. Ununuzi na a) Uhakiki wa usalama wa lakiri na kiasi cha dhahabu uthaminishaji wa madini iliyotengwa kuuzwa Benki Kuu ya Tanzania au katika viwanda vya kusafisha dhahabu utafanywa na Tume ya Madini wakati wa uwasilishaji kwenye viwanda vya kusafisha dhahabu; b) Dhahabu iliyotengwa itasafishwa kwa ajili ya kupata zao la mwisho (refined gold) pamoja na madini ambata; Cc) Mmiliki wa leseni ya uchimbaji wa madini, mfanyabiashara mkubwa wa madini, Ofisi ya Afisa Madini Mkazi na Benki Kuu ya Tanzania i watapokea taarifa ya matokeo ya mwisho ya viwango vya madini baada ya dhahabu kusafishwa; d) Mnunuzi wa dhahabu iliyotengwa kwa mujibu wa sheria (Benki Kuu ya Tanzania au kiwanda cha kusafisha dhahabu) atafanya malipo kwa mmiliki wa madini kwa kuzingatia taarifa ya mwisho iliyotolewa na kiwanda cha kusafisha dhahabu nchini; e) Umiliki wa madini utahama kutoka kwa mmiliki wa leseni ya uchimbaji wa madini au mfanyabiashara mkubwa wa madini kwenda kwa Benki Kuu ya Tanzania au kiwanda cha kusafisha dhahabu baada ya kukubaliana kusafisha madini hayo na malipo yake kukamilika; na f) Uhakiki wa kiasi na ubora wa dhahabu iliyosafishwa utafanywa na Tume ya Madini pamoja na mmiliki mpya wa Madini hayo (Benki Kuu ya Tanzania au Kiwanda cha kusafishia dhahabu) mbele ya wawakilishi wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama na Mamlaka ya Mapato Tanzania wakati wa kufunga madini kwa ajili ya kusafirisha nje au ndani ya nchi.

  3. 3. Utaratibu wa utengaji na a) Wachimbaji wakubwa na kati wa dhahabu malipo ya mrabaha wa watatenga kiwango cha dhahabu wakati wa madini yanayouzwa ufungaji wa madini (boring) kwa kila uzalishaji ndani ya nchi unaofanyika kabla ya kusafirishwa nje ya nchi na yatalipiwa mrabaha stahiki; 4 <!-- page 6 --> MHE WONGOZO te b) Iwapo dhahabu inatoka kwenye mitambo ya uchenjuaji (Elution plants, CIP 8 CIL), mmiliki atatenga kiwango cha dhahabu kabla ya kupeleka kwenye soko la madini kwa kila uzalishaji unaofanyika, kwa ajili ya kuuzwa kwa wafanyabiashara wakubwa au kusafirisha nje ya nchi na kitalipiwa mrabaha stahiki; Cc) Wafanyabiashara wakubwa watakaonunua dhahabu kutoka kwenye vyanzo vingine vya uzalishaji (Mitambo midogo ya uchenjuaji madini na wachimbaji wadogo) na kuuzwa kwenye masoko ya madini watawajibika kutenga kiwango cha madini kwa kila ununuzi unaofanyika kabla ya Afisa Madini wa eneo husika kutengeneza kumbukumbu namba za malipo za tozo stahiki za Serikali. Ofisi ya Afisa Madini Mkazi itafanya uhakiki wa malipo ya mrabaha wa asilimia nne (4%) na sita (6%) kwa mujibu wa Sheria kabla ya madini kusafirishwa nje ya nchi; na d) Benki Kuu ya Tanzania haitatozwa ada, tozo, kodi na malipo mengine yoyote kwa kuwa imeondolewa wajibu huo kwa mujibu wa Kifungu cha 22 cha Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania, Sura 197. Umetolewa, Eng. oo M. Lwamo KAIMU KATIBU MTENDAJI TUME YA MADINI 5

Mwongozo wa Ununuzi wa Dhahabu (Toleo la Agosti 2024) with covering minute · Nelum